RAIS MAGUFULI AENDELEA NA UTEUZI,LEO AWATEUA HAWA,SOMA HAPO KUJUA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli, leo tarehe 16 Januari, 2017 amefanya uteuzi wa Wabunge
wawili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Balozi mmoja.
Wabunge walioteuliwa ni Alhaji Abdallah Majula
Bulembo na Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi.
Wabunge wateule hawa wataapishwa kwa taratibu za
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Abdallah Bulembo ndiye mwenyekiti wa Jumuiya ya
Wazzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), na pia alikuwa ni mujumbe wa Bunge Maalum
la Katiba, kabla ya majukumu ya kuendesha kampeni za urais mwaka 2015
zilizomuingiza Rais Magufuli madarakani.
Kwa upande wake Prof Kabudi, ni mhadhiri wa Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Sheria, lakini kilichong'arisha zaidi ni
pale alipoteuliwa na Rais Kikwete kuwa mmoja kati ya wajumbe wa Tume ya
Kukusanya na Kuratibu Maoni ya Katiba, iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Jaji Mst.
Joseph Sinde Warioba.
Prof. Kabudi amekuwa mahiri katika mihadhara
mbalimbali kitaifa, hasa wakati ule wa mchakato wa Katiba Mpya.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Benedicto
Martin Mashiba kuwa Balozi.
Kituo cha kazi na tarehe ya kuapishwa kwa Balozi
Mteule Benedicto Martin Mashiba itatangazwa