TUNDU LISSU ACHARUKA SASA,AIBUKA NA KUAAPA KUPAMBANA MPAKA MBUNGE WA CHADEMA ALIYEFUNGWA ATOKE,SOMA HAPO KUJUA
HATUA ya Mahakama ya Wilaya ya Kilombero, Morogoro
kumfunga Peter Lijualikali, Mbunge wa Jimbo la Kilombero miezi sita jela,
inatokana na visa vya kisiasa, anaandika Pendo Omary.
Ni
kauli ya Tundu Lissu, Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) leo mbele ya waandishi wa habari aliokutana nao kwenye Makao Makuu ya
chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki amesema
kuwa, vita kati ya upinzani na Chama Cha Mapinduzi (CCM) vimesababisha
Lijuakali (Chadema) kupata hukumu hiyo ya kisiasa.
Mbele ya waandishi wa habari Lissu amesema kuwa,
“hiyo ni hukumu ya kisiasa” na kwamba, Jeshi la Polisi nalo limeingizwa kwenye
vita hivyo.
Lissu amesema, chanzo cha hukumu hiyo kinatokana na
mgogoro wa uongozi ndani ya Halmashauri ya Kiliombero ambapo Chadema na
washirika wake wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) walishinda
madiwani wengi.
Hivyo, kwa mujibu wa Lissu, Halmashauri ya
Kailombero ilipaswa kuongozwa na mwenyekiti anayetoka na Ukawa na awe Chadema.
“Ili hilo lisiwezekane, na ili CCM wachukue
Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero licha ya kushidwa kwenye udiwani, ilibidi
wamfanyie Lijualikali mambo ya ajabu,” amesema Lissu
Lijualikali (30) amehukumiwa jana kwa kosa la
kufanya fujo na kusababisha taharuki. Huku Stephano Mgata (35), Dereva wake
ambaye ni mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo akifungwa kifungo cha miezi sita
nje.
“Kifungo cha Mh. Lijualikali ni adhabu ya kisiasa.
Mh Lijualikali ni mfugwa wa kisiasa. Amefugwa kwa sababu ya siasa.
“Adhabu ya kisisa ni vita ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM) dhidi ya Chadema na wanatumia Jeshi la Polisi, wanatumia mahakama na
kwingineko. Vita hii hii wanawatumia akina Lipumba (Profesa Ibrahim Lipumba,”
amesema Lissu na kuongeza;
“Kwingine wamemweka Lema (Godbless Lema, Mbunge wa
Arusha Mjini) mahabusu kwa miezi mitatu. Hakuna jinai yoyote. Tuliwashinda
kwenye uchaguzi.
“Sasa baada ya uchaguzi walimfungulia Lijualikali
kesi ya kupinga matokeo mahakama kuu, tukawapiga chini. Wamefungua rufaa na
tunawatandika.”
Mwanasheria huyo amesema kuwa, nchi hii ina wafungwa
wa kisiasa na kwamba, pamoja na CCM kudhani kwamba, kumfungulia kesi Lijuakali
kutawapa afueni. Wasahau.
“Tuna wafungwa wa kisiasa nchi hii. Wale
wanaofikiria kwamba kumfunga Lijualikali CCM itapendwa na wananchi wa kilombelo
wasahau hilo.
“Huwezi kuwatesa wananchi, ukatesa viongozi
waliowachagua kwa mapenzi yao halafu ukategemea wakupende. Wasahau,” amesema
Lissu.
Aidha, Lissu ametoa ufafanuzi kuwa Ibara ya 67 ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inamlinda Lijualikali hivyo hawezi
kupoteza ubunge wake kutokana na hukumu hiyo.
Amesema Chadema hakijaridhika na hukumu hiyo, hivyo
kwa sasa wanaandaa utaratibu wa kisheria ili kukata rufaa kuipinga ambapo hatua
hiyo inaweza kuchukua siku mbili kukamilika.
Timothy Lyon, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo alisema,
amemhukumu Lijualikali baada ya kumtia hatiani kwa kosa yeye na dereva wake na
kwa kuwa, mbunge huyo alipatikana na hatia katika kesi tatu huko nyuma na
kuhukumiwa kulipa faini hivyo alistahili kutumikia adhabu hiyo.
Kesi zilkizotajwa na Lyon zinazomuhusu Lijualikali
ni namba 338, namba 220 na namba 340 zote za mwaka 2014.
Katika kesi hiyo, Dotto Ngimbwa, Inspekta wa Polisi
aliiambia mahakama kuwa, Lijuakali akiwa mshtakiwa namba moja pamoja na Mgata
walitenda kosa hilo Machi Mosi mwaka 2016 eneo la Kibaoni katika ukumbi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Kialombero na kwamba, walifanya fujo kinyume cha
sheria.
Alisema tukio hilo lilitokea Machi Mosi mwaka huo
saa 4 asubuhi ambapo washtakiwa walikana mashtaka lakini upande wa mashtaka
ukathibitisha bila kuacha shaka kwamba, walitenda kosa.