TAASISI YA TICHER JUCTION YAWAPIGA MSASA WALIMU,SOMA HAPO KUJUA
Walimu nchini wametakiwa kujitadhimini ili kujua
mbinu za kufundishia ili waweze kuwapa mafunzo bora wanafunzi
Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam,!Afisa
Mradi wa Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya TicherJuction,Njama Salum wakati
akitoa mafunzo kwa walimu mbali mbali nchini yenye lengo la kuwapa walimu mbinu
za kufundishia pindi wawapo shuleni.Taasisà hiyo ambayo imekuwa ikihusika
katika kuwajengea uwezo kwa walimu pindi wamalizapo vyuoni waweze kupata kazi.
Amesema licha ya walimu kumaliza vyuo mbali
mbali,lakini bado walimu wamekosa mbinu ya kufundishia wanafunzi jambo analodai
limepelekea waajiri kushÃndwa kuajiri walimu hao.
Njama amezitaja mbinu hizo ni pale mwalimu kushindwa
kuweza kusimama kwenye darasa wakati wa kufundisha ,pia wengi wao
kushindwa kutoa uwezo wake na kupeleka kwa mwanafunzi.
Amesema baada ya taasisi hiyo kubaini changamoto
hizi kwa walimu ndio ikawafanya kuandaa mafunzo hao ili kuwakomboa walimu.
Hata hivyo,Njama ameitaka serikali itunge mtaala
ulio sahihi ili kumfanya mwalimu aweze kupata ajira.