CHAMA CHA CUF CHALIA NA RAIS MAGUFULI,WADAI NDIO KIKWAZO CHA KUFANYA BIBAYA KWENYE UCHAGUZI MDOGO,SOMA HAPO KUJUA

NA KAROLI VINSENT
Chama cha Wananchà (CUF) kimesema katazo la Rais John Magufuli kutoruhusu
mikutano ya siasa pamoja na Nguvu kubwa inayotumiwa na vyombo vya dola kwa
vyama vya upinzani ndio sababu iliyochangia
chama hÃcho kufanya vibaya kwenye uchaguzi mdogo uliomalizika hivi karibuni .
Ambapo katika uchaguzi huo mdogo uliofanyika januari
22,Chama Cha Mapinduzi CCM kilishinda Kata 19 kati ya kata 20 za udiwani pamoja
na kushinda jimbo moja Dimani ,huku Chama cha demokrasia Chadema kimeambulia
kata moja huku chama cha Cuf hakijaambulia hata kata moja.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es
Salaam,Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Cuf,Abduri Kambaya(Pichani),wakati
akitoa tathmini ya uchaguzi huo,
Ambapo amesema kitendo cha Rais Magufuli kukataza
mikutano hiyo kimekiathiri chama hicho,amedai kuwa pindi walipokwenda kupiga kampeni kwenye kata
hizo wameonekana wageni,
Amedai kuwa Chama cha CCM kinatumia mwanya huo kushinda
katika uchaguzi huo.
Mbali na sababu hiyo,pia Kambaya ameitaja sababu
iliyopelekea chama hicho kufanya vibaya ni matumizi ya nguvu ya vyombo vya dola
kwa vyama vya upinzanà ikiwemo kuwakamata viogozi wake jambo lilowatisha wapiga
kura
Post Comment