Zinazobamba

KAMPUNI YA MZURI AFRIKA NA GRAMI AFRIKA YALETA SULUHISHO SEKTA YA KILIMO NCHINI TANZANIA.


Na Mussa Augustine 

Kampuni ya Mzuri Afrika na Grami Afrika imeleta mashine ambayo inatumika katika kurahisisha shughuli za kilimo cha mazao ya nafaka,na kumsaidia mkulima kupata mazao mengi wakati wa mavuno.

Mashine  hiyo imetengenezwa  nchini Poland kutoka Kampuni mama ya Mzuri World inayotengeneza teknolojia za kisasa za  kilimo,ambapo Mashine iliyoingizwa nchini Tanzania inauwezo mkubwa wa kuleta Mapinduzi chanya kwenye sekta ya kilimo.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Machi 7,2025 Jijini Dar es salaam Mkurugenzi  Mkuu wa Kampuni ya Mzuri Afrika na Grami Afrika Bw.Shaaban Mgonja amesema kwamba Teknolojia ya Mzuri imekua ikifanya vizuri hata kwenye nchi za Magharibi akitolea mfano nchini Ukraine ambapo wanatumia teknolojia hiyo na kuweza kuzalisha ngano kwa asilimia 30.

" Mashine hii ya Mzuri inafanya kazi  kwa wakati mmoja,yaani kutifua na kulegeza udongo, kuweka mbolea,pamoja na  kupanda,hivyo inatofautiana na teknolojia ya plau inayotumika kwa sasa  ambayo inamfanya mkulima atumie muda mrefu shambani pamoja na kutumia mbolea nyingi". amesema Mgonja

Nakuongeza kuwa" mashine hii ya Mzuri inauzwa kiasi cha shingi milioni  mia nne(400,000,000)gharama ambayo wakulima wadogo  hawawezi kuimudu,Mashine hii inafaa kwa wakulima wenye mashamba makubwa kwani wanalima mazao mengi wanapata faida kubwa ya kuweza kumudu gharama za kulipia mashine hiyo."
Aidha Mgonja amendelea kusema kuwa kwa sasa Kampuni hiyo imefanya mazungumzo na Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kuweza kusambaza teknolojia hiyo Nchini Tanzania,nakwamba  tayari imeanza kushirikiana na Chuo Kikuu  Cha Kilimo Morogoro( SUA) kwa ajili ya kutoa Mafunzo kuhusu matumizi ya  teknolojia hiyo.

Pia amesema kuwa  kampuni hiyo imeanzisha shamba darasa katika eneo la Vigwaza  Mkoani Pwani ili kuwasidia wakulima kupata elimu bure kwa vitendo kuhusu matumizi ya Mashine  hiyo pamoja na matumizi ya Mbolea inayozalishwa na kampuni tanzu ya Grami Afrika ambayo imezalisha aina 11 za mbolea nakwamba aina 9 ya mbolea hizo  tayari zimesajiliwa nakuanza kutumika.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mzuri World iliyopo Nchini Poland,ambayo ni watengenezaji wa teknolojia hiyo Marek Rozniak amesema kuwa teknolojia hiyo kwa sasa inatumika katika nchi 50 Duniani ikiwemo Tanzania ,huku akidai kuwa imekua ikisaidia kuzalisha mazao mengi kutokana na teknolojia hiyo kufanya kazi kwa pamoja ya kutifua na  kulainisha udongo,kuweka mbolea na kupanda mbegu,kwa muda mfupi.

"Mashine ya Mzuri yenye Mita 3 ambayo ndiyo tumeileta Tanzania inauwezo wa kulima hekari 7 kwa saa moja,na inahudumiwa na watu wawili tu,na ukitumia Mashine hii vizuri unaweza kupata mazao zaidi ya tani 12, na hili linawezekana kwa wakulima wa mazao ya nafaka hapa Tanzania" amesema Marek
Hata hivyo mataalamu muelekezi katika zana za kilimo Kampuni ya Mzuri Mhandisi Richard Shetto amefafanua kuwa matumizi ya Mashine ya Mzuri inasaidia  kutengeneza mifereji ambayo maji ya mvua yanapata nafasi ya kupenya mpaka chini kiasi cha kwamba yanaweza kunyonywa na mimea,lakini pia kuvunja "jasi"ambayo inazuia mizizi ya mimea kwenda chini nakufanya mimea kudumaa nakutoa mazao kidogo.

"Katika nchi ambazo wanatumia mashine hii ,ukiangalia sisi kwa kilimo cha plau,mfano mkulima akilima mahindi hata kama akitumia mbolea atafikisha gunia kumi na tano(15) ishirini kwa sehemu zenye mvua nyingi,lakini akitumia mashine za mzuri anaweza kupata hadi magunia arobaini (40) kwa hekari moja" amesema Mhandisi Shetto

Nakuongeza kuwa,"hii mashine ya Mzuri inafanya kazi tatu kwa mpigo,kuweka mfereji kutifua kidogo kwenye mfereji,kuweka mbegu,na kuweka mbolea,na uwekaji wake wa mbolea hua ikiwekwa kidogo chini ya mbegu,kwahiyo matumizi ya Mbolea yatapungua kwa karibu ya theluthi kwani mbolea itakua inatumika tu sehemu inapohitajika.
Kampuni ya Mzuri Afrika na Grami Afrika imekua ikitengeneza zana mbalimbali za kilimo pamoja na Mbolea,ambazo zinatumika katika nchi mbalimbali za Afrika na kuleta matokeo chanya katika kuwainua wakulima kiuchumi kupitia sekta ya Kilimo.



Hakuna maoni