SERIKALI YAWAKUMBUKA WATUMISHI WA UMMA KIMTINDO,YAWAPA MIKOPO YA NYUMBA,SOMA HAPO KUJUA
Mkurugenzi wa Idara ya Nyumba Wizara ya Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Bw. Michael
Mwalukasa akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Jijini Dar es salaam kuhusu mfuko wa kuwawezesha watumishi
wa Serikali kumiliki Nyumba ambapo zaidi ya watumishi 2000 wameshanufaika na mikopo
yenye riba nafuu ya asilimia 3 ili
kuwawezesha kumiliki nyumba bora. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Mikopo ya Nyumba
Bi Lucy Kabyemera na Kushoto
|
Wizara ya ardhi,nyumba na maendeleo ya Makazi
kupitia idara ya nyumba imepewa jukumu
la kusimamia mfuko wa mikopo ya Nyumba kwa watumishi wa serikari kwa lengo la
kuwawezesha watumishi wake kujenga,kununua au kukarabati nyumba kupitia mkopo
huo mwenye masharti
nafuu.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Idara ya nyumba Michael Mwalukasa amesema kuwa mfuko huu ulianzishwa kwa ajili ya kusaidia na kuwawawwzesha watumishi wa serikali wanaoishi mjini na vijijini kupata mkopo wa nyumba wenye masharti nafuu
kwa ajili ya kujenga au kununua nyumba.
Ameongezakuwa mfuko huo unatoa mikopo kuanzia milioni 20 kwa riba ya asilimia tatu ambao muda wa juu wa kurejesha mkopo huo ni miaka thelasini(30) katika kipindi cha utumishi kabla ya kustaafu au anapoacha utumishi kwa sababu zozote zile.
Mwalusakaamesema kuwa kuna sifa mbalimbali za kupata mkopo huu ikiwa ni pamoja na mkopaji ni lazima awe mtumishi wa serikali, raia wa Tanzania,aliyeajiriwa kwa masharti ya kudumu na kuthibitishwa kazini pamoja na kuwa na hati ya kiwanja ambacho kitamuwezesha kupata mkopo kwa
ajili ya kujenga.

Kwa upande wake Mkurugenzi msaidizi mikopo ya nyumba Lucy Kabyemera ameeleza faida za mikopo hiyo kwa watumishi wa serikali ikiwa ni pamoja na kuwawezesha watumishi
kupata mikopp yenye riba nafuu, kuweza kumiliki nyumba kwenye maeneo yenye hadhi,kuchochea kasi ya maendeleo kwenye miji na wilaya mbalimbalipamoja na kutoa fursa kwa watumishi kumiliki nyumba kwa kadri ya matakwa yao.
"Faida zipo nyingi sana kwani pamoja na kunufaika na mikopo baadhi ya wakopaji pia wameendelea kunufaika na ushauri wa kutumia technologia ya bei nafuu ya ujenzi
kutokana na tafiti zilizofanywa na taasisi iliyopo chini ya Wizara
(NHBRA)."
Kabyemera ameongeza kwa kusema kuwa
ujenzi wa nyumba unahitaji gharama nyingi hivyo ndio maana wameamua kutoa mikopo hasa kwa watumishi wa serikali ili iweze kuwasaidia kwa kuwapa fedha taslimu ya shilingi milioni 20.
Mfuko wa Mikopo ya Nyumba ni moja wapo ya vyombo vilivyoanzishwa na serikali mara baada ya nchi kupata uhuru mnamo mwaka 1963 kupitia waraka wa watumishi wa serikali na.8 na badae kuendeshwa kupitia waraka wa
watumishi wa serikali na.4 wa mwaka 1965.