Zinazobamba

JESHI LA POLISI DAR LAUA MAJAMBAZI WATATU,WAPO WALE WALIOIBA MILIONI 25 KARIBIA YA OFISI ZA GAZETI LA SERIKALI,SOMA HAPO KUJUA






WATU watatu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wameuawa katika shambulio la kutupiana risasi na Askari Polisi walipokuwa wakitaka kufanya tukio la ujambazi maeneo ya Mikocheni, Jijini Dar es salaam jana

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro, amesema watu hao wanaodaiwa kuwa majambazi inadaiwa walifanya tukio la unyanganyi juzi maeneo ya Tazara ambapo waliondoka na sh.milioni 26.

Kamanda Sirro, amesema watu hao walikuwa wanne ambapo watatu waliuawa wakati wakirushiana risasi na polisi.

Amesema watu hao walikuwa wakifanya tukio la ujambazi kwa kutumia pikipiki ambapo katika tukio hilo mmoja alitoweka na usafiri huo.

Sirro amesema ndugu zao kama wanawatafuta polisi watatoa msaada wa kupeleka miili yao ili waweze kuhifadhi.

Katika matukio mengine, Jeshi la Polisi limewakamata vijana wanne wanadaiwa kufanya wizi wa vitu mbalimbali ikiwe  Computa, ving'amuzi katika ofisi ya mpiga chapa mkuu wa serikali, walikamatwa na hakuna mahusiano ya wafanyakazi wa ofisi hiyo kuhusika katika tukio hilo.
Wakati huo huo jeshi la Polisi linamshikilia Mlinzi wa Kampuni ya Ulinzi ya Amadori, Anwaz Ally (45) aliyekutwa na silaha ya moto katika sehemu ya maungo ya mwili wake aina ya berretta na risasi 23 huku akiwa hana kibali cha umiliki wa silaha hiyo.


Aidha Polisi inamshikilia mtu mmoja anayedaiwa  kufanya uhalifu kwa watalii waliokuwepo Wilaya ya Mkuranga na kuchukua vitu mbalimbali na upelelezi unaendelea kutafuta mtandao huo