MGOMBEA WA URAIS WA KWANZA MWANAMKE NCHINI KUAGWA JUMAMOSI,SOMA HAPO KUJUA
Na Anthony John, Globu ya Jamii
MWILI wa aliyekuwa Mgombea wa Urais Mwanamke kupitia Chama Cha PPT Maendeleo Dkt, Anna Senkoro ambaye alikuwa mgombea wa Urais mwanamke wa kwanza nchini kwenye uchaguzi wa mwaka 2005 unatarajiwa kuagwa Jumamosi katika kanisa la Winner Chaapel International lililopo Ukonga Jijini Dar es salaam majira ya saa saba mchana na ibada itakayoongozwa na Mchungaji Samuel Adeyemi.
Akizungumza leo na waandishi wa habari katika makazi ya marehemu huyo Tabata jijini Dar es Salaam ,Mdogo wa Marehemu George Nathaniel amesema baada ya kumaliza ibada ya kuagwa mwili huo utaapelekwa katika Makaburi ya Kinondoni kwa ajili ya mazishi.
Nae Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Ukonga, Dkt Makongoro Mahanga amesema ameupokea msiba huo kwa masikitiko makubwa ya kuondokewa na mwanaharakati wa siasa na kuwaomba wana familia kushirikiana katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Makongoro, amesema marehemu Dkt. Anna alikuwa mfano wa kuigwa katika jamii kwa uhodari wake.Aidha mtoto wa pili wa marehemu Joan Senkoro amesema bado wataendelea kumuombea mama yao kwa Mungu na amejifunza mengi ikiwemo msimamo aliokuwa nao mama yake.

Aliyekuwa Mbunge wa Ukonga, Dkt. Makongoro Mahaga akizungumza katika Msiba wa aliyekuwa Mgombea wa Uraisi wa Chama cha PPT Maendeleo,Dkt.Anna Senkoro leo jijini Dar es Salaam |
Sehemu ya waombolezaji waliofika katika Msiba wa aliyekuwa Mgombea wa Uraisi wa Chama cha PPT Maendeleo, Dkt.Anna Senkoro, leo jijini Dar es Salaam. Picha na Bakari Madjeshi wa Globu ya Jamii. |