AMUUA MKEWE KWA NYUNDO KISA WIVU WA MAPENZI,SOMA HAPO KUJUA
Mwanamke mmoja mkazi wa Mikumi wilayani Keya, Mbeya
aliyefahamika kwa jina la HILDA SIGARA amefariki dunia akiwa anapelekwa
Hospitali kwa matibabu baada ya kupigwa nyundo kichwani na mume wake aitwaye
REBSON TWEVE umri kati ya miaka 30 – 35
Kamanda wa polisi mkoani humo DCP Dhahiri
Kidavashari amesema tukio hilo limetokea mnamo tarehe 05.01.2017 majira ya saa
12:00 asubuhi ambapo imedaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi
kwani inasadikiwa mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu marehemu kuwa ana mahusiano ya
kimapenzi na mwanaume mwingine.
Amesema katika eneo la tukio kumekutwa nyundo moja,
kisu kimoja na fimbo ya muanzi ambavyo vinasadikiwa kutumika katika tukio hilo.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Wilaya
Kyela ukisubiri kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu na upelelezi unaendelea huku
mtuhumiwa akiwa ametoroka mara baada ya tukio na juhudi za kumtafuta
zinaendelea.
Aidha, katika matukio mengine kamanda huyo amesema
kuwa jeshi la polisi limepokea taarifa za kujinyonga kwa watu wawili ambao
miili yao imekutwa ndani ya nyumba zao katika maeneo tofauti.
Watu hao ni pamoja EDWARD PETER mfanyabiashara
na Mkazi wa Majengo na aliyekutwa amekufa chumbani kwake huku mwili wake ukiwa
hauna majeraha yoyote, na mwingine ni ROBERT MWAISENYE Mkazi wa Mbugani
wilayani Chunya ambaye alikuwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya manila akiwa
ndani ya nyumba yake.