SERIKALI YA MAGUFULI YACHARUKA,NI KUHUSU BEI MPYA UMEME,SOMA HAPO KUJUA
Taarifa ya kusitisha kwa bei hiyo ilitolewa jana na
Profesa Muhongo kupitia barua yake kwa Ewura.
Muhongo amesema kuwa amesitisha bei hiyo mpya
kwa sababu nne, ikiwamo kutoshirikishwa katika mchakato huo akiwa ni waziri
mwenye dhamana.
“Ewura walipokwenda mikoani Watanzania
wote walipinga bei kupanda, wao wametumia kigezo kipi cha kupandisha? Pili
taratibu zilizopo ni kwamba Tanesco wanapeleka maombi Ewura, kisha Ewura
wanafanya zoezi hilo la kuuliza wahusika watumiaji wa umeme, baada ya hapo
wanatengeneza ripoti wanaileta wizarani, na ningaliipata hiyo ripoti.
“Hivi tunavyoongea sijaipata mkononi,
nikiipata nitaiita Ewura na Tanesco tunajadili na baada ya hapo ndipo wanaenda
kutangaza. Wao wametangaza hata mimi taarifa nazipata kama wewe,” alisema
Profesa Muhongo.
Katika sababu ya tatu ya kusitisha bei hiyo, Profesa
Muhongo alisema hakuna ukweli kuwa kupandisha bei ya umeme kutasababisha
Tanesco imalize matatizo yake kifedha.
“Tanesco kila mwaka inapandisha bei,
mbona hawajajikwamua? Mbona madeni yanazidi kuongezeka? Nyingine ni kwamba
tunakopa fedha kutoka nje ya nchi na watakaolipa hilo deni ni Watanzania wote,
sasa hatuwezi kukopa kulipa madeni ya Tanesco halafu shukrani tutakayoipata ni
kupandishiwa bei ya umeme tena.
“Nyingine nenda ufuatilie Tanesco wana
matumizi mabaya ya fedha, nimesitisha zoezi lao, sijui kama hizo fedha
wamerudisha, unajua wanapeana wale walioko juu bonasi kati ya Sh milioni 40 na
milioni 60 kwa mwaka,” alisema Profesa Muhongo.
Alisema Ewura wanapaswa kupeleka ripoti ijadiliwe,
kwani haiwezi kuwa Serikali ndani ya Serikali na haiwezi kupandisha bei bila
waziri mwenye dhamana kujua kwa kuwa inapata bajeti kutoka bungeni.