HIVI NDIVYO ZITTO KABWE ALIVYOWAJIBU WABUNGE WENZAKE WALIOPINGA KUTAJA MSHAHARA WAKE,SOMA HAPO KUJUA
December 30 2016 mbunge wa kigoma mjini na
kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe alitoa taarifa kuhusu
madeni anayodaiwa, kiwango cha mshahara wake wa mwaka, kiasi cha pesa kilichopo
benki, posho pamoja na mali zote anazomiliki.
Kupitia ukurasa wake wa facebook ametoa ufafanuzi
akidai baadhi ya wabunge wenzake hawajafurahishwa namna alivyoweka na hivyo
ameeleza kuwa….
Mshahara wa mbunge kwa mwezi ni tshs 4.6 milioni
kabla ya kodi, baada ya kukatwa kodi ya mapato mbunge hubakia na tshs 3.2
milioni kwa mwezi. Hivyo Mshahara ni tshs 38.4 milioni kwa mwaka.
Mbunge hulipwa pia tshs 8.2 milioni kila mwezi kama
posho ya kazi za Ubunge (mafuta ya kutembelea Jimbo, matengenezo ya gari,
malipo ya watumishi wa Ofisi ya Mbunge kama vile Dereva, mhudumu wa ofisi na
Katibu wa Mbunge). Hii ndio inapelekea mapato ya jumla ya tshs 99 milioni kwa
mwaka niliyoweka kwenye taarifa ya rasilimali na madeni.
Mbunge pia hulipwa posho za kujikimu na posho za
vikao ( kwa wale wanaochukua posho hizi). Hizi hutolewa kulingana na mahudhurio
ya vikao.
Aidha zitto ameongeza kuwa kuweka wazi tamko la mali
na madeni kwa sasa sio takwa la kisheria bali ni uamuzi binafsi wa Mbunge ama
Kiongozi mwengine wa umma.
"Mimi ninatakiwa na katiba ya chama changu
kuweka wazi tamko la mali na madeni kwa mujibu wa azimio la Tabora linalohuisha
azimio la Arusha.
" Hivyo, ichukuliwe kuwa kuweka kwangu wazi
tamko husika ni kutekeleza matakwa ya katiba ya chama ambacho Mimi ni
mwanachama na sio kuwashtaki wenzangu kwa wananchi. Mimi naamini kwamba uwazi
ni moja ya silaha madhubuti ya kupambana na ufisadi. Nimewasilisha muswada
bungeni kutaka uwazi huu liwe sharti la sheria za nchi yetu"- Zitto