Zinazobamba

NAIBU MEYA WA UKAWA ILALA AZIDI WAJALI WAPIGA KURA WAKE,SOMA HAPO KUJUA

Naibu meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti, Omary Kumbilamoto akiwa amekalia Cherahani mara baada ya kuikabidhi kwa kikundi cha wajasiliamali wa mtaa wa ukombozi vingunguti.

NAIBU Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti, Omary  Kumbilamoto amesema maisha ya watu wa vingunguti na uchumi wao inategemea pesa za biashara ya mbuzi.


Akizungumza na wakazi wa Vingunguti katika mkutano wa hadhara wa kueleza mambo aliyofanya ndani ya mwaka mmoja Kumbilamoto ametaja kuwa bila ya mbuzi vingunguti itakuwa maskini.

“nimejitahidi kutatua tatizo la wafanya biashara wa mbuzi ambao walitakiwa wahamishwe kupelekwa Pugu kwa kuangalia maslahi na vipato vya wakazi wa Vingunguti kuwa biashara hiyo itabaki vingunguti na itaendelea kama kawaida". amesema  Kumbilamoto.

Katika kipindi cha mwaka mmoja ambapo lengo lilikuwa kutoa shukrani, Kumbilamoto hakusahau Nyanja nyingine nyeti ikiwemo nyanja ya Afya ambapo alijitahidi kuwapatia Ambulance moja katika Hospitali ya Vingunguti ambayo ameahidi kuwa  mali ya wakazi wa  eneo hilo.

Pia hakuacha Elimu ambapo alisaidia shule ya Sekondari Miembeni kuchangia kupatikana kwa Umeme, hivyo wanafunzi kusoma bila matatizo , mambo mengine ambayo ameyagusia na kuyatolea ufafanuzi  ni pamoja na Sekta ya michezo, alitoa Mashine mbili za kufulia mashuka katika Hospitali hiyo, aliweza kushugulikia bomoa bomoa  na haki ya wafanyabiashara katika machinjio ambapo damu ilikuwa inapotea kwa wenye haki hawapati haki hiyo hivyo yeye amelishughulikia na limekaa sawa.

Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti, Omary Kumbilamoto akihutubia wakazi wa vingunguti katika mkutano wa hadhara.