LOWASSA ANAWANANGA WALIOMTABILIA KIFO,ASEMA YUPO KAMILI,SOMA HAPO KUJUA
Waziri Mkuu aliyejiuzuru Edward Lowassa, amesema
kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ina watu wenye roho mbaya kwani
waliwahi kumuombea kifo,lakini hadi leo anadunda.
Lowassa ambaye alikuwa mgombea urais wa Chadema na
kuungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi(Ukawa), amesema
baadhi ya waliomwombea kifo leo hawapo duniani,kwani mungu ndiye anayepanga
maisha ya mwanadamu.
“Kule kwa wenzetu kuna watu wenye roho
mbaya,kwani hata mimi waliniombea kifo,waliniombea kifo muda mrefu kweli lakini
mpaka sasa bado nadunda tu wakati baadhi ya walioniombea hivyo,leo hawapo
duniani kwa mapenzi ya mungu”alisema Lowassa.
Lowassa aliyasema hayo jana baada ya wananchi
waliokuwa kwenye mkutano wa ufunguzi wa uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya
Matevezi jimbo la Arumeru Magharibi,kupaza sauti wakimuuliza juu ya hatima ya
mbunge wao Lema ambaye yupo Gereza la kisongo kwa miezi miwili sasa.
Katika hatua nyingine, Lowassa aliwataka timu
ya kampeni na wananchi kuhakikisha kura haziibiwi kwa kile alichoeleza kuwa
Chadema ina nguvu.