BADILIKO MAKUBWA JESHI LA MAGEREZA NCHINI,MAOFISA WAKE WABADILISHWA KILA ENEO,SOMA HAPO KUJUA
Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini,
Dkt. Juma Ally Malewa(pichani) amefanya Mabadiliko ya Uongozi kwa baadhi ya
Wakuu wa Magereza Mikoa na vituo mbalimbali hapa nchini.
Mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa
Magereza Mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza SACP Katos
Rugainunura amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza sehemu ya Utawala na nafasi
yake inakaimiwa na Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Mzee Nyamka aliyekuwa Mkuu
wa Utawala Magereza Mkoani Morogoro.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza SACP
Antonino Kilumbi aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma amehamishwa kwenda
Makao Makuu ya Magereza kuwa Mkuu wa Kikosi cha Ujenzi na nafasi yake
inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza SACP Julius Sang’udi
aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mbeya.
Aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro
Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Anderson Kamtiaro anaenda kuwa Afisa Mnadhimu
Magereza Mkoani Arusha na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa
Magereza ACP Hassan Mkwiche ambaye alikuwa ni Mkuu wa Gereza Kuu Karanga, Moshi.
Aliyekuwa Mkuu wa Gereza Same Kamishna Msaidizi wa
Magereza ACP Evarist Katego anakwenda kuwa Mkuu wa Gereza Kuu Karanga, Moshi.
Aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mwanza Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Magereza SACP Uwesu Ngarama amehamishiwa Makao Makuu kuwa Boharia Mkuu wa Jeshi
na nafasi yake inachukuliwa na aliyekuwa Afisa Mipango wa Jeshi ACP Athuman
Kitiku.
Aidha, aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoani Mtwara,
Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Musa Kaswaka anakwenda Makao Makuu Kitengo
cha Ukaguzi na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP
Ismail Mlawa aliyekuwa Mkuu wa Kiwanda cha Samani Gereza Kuu Ukonga. Aliyekuwa
Afisa Mdhibiti wa Fedha wa Jeshi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza SACP
Gideon Nkana anakwenda kuwa Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga,
Dar es Salaam na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP
Chacha Jakson.
Wengine ni pamoja na aliyekuwa Afisa Mnadhimu wa
Magereza Mkoa wa Mbeya ACP Kijida Mwakingi anakaimu nafasi ya Mkuu wa Magereza
Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Abdalah Misanga anayetoka
Gereza Mgumu kwenda kuwa Mkuu wa Gereza Msalato, Kamishna Msaidizi wa Magereza
ACP John Itambu anayetoka Gereza Kilosa kwenda kuwa Mkuu wa Kiwanda cha Samani
Gereza Kuu Ukonga.
Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Erasmus Kundy
anayetoka Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Ukonga kwenda Makao Makuu Kitengo
cha Habari, Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Julius Ntambala aliyekuwa Mkuu wa
Kitengo cha Ujenzi Makao Makuu anabakia Makao Makuu Kitengo cha ujenzi kuwa
Msaidizi wa Mkuu wa Kitengo, Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Sylivester Mrema
anayetoka Gereza Idete kwenda Gereza Ubena kuwa Mkuu wa Gereza.
Aliyekuwa Mkuu wa Gereza Ubena Kamishna Msaidizi wa
Magereza ACP Shaba Zephania anakwenda Magereza Mkoa wa Pwani kuwa Afisa
Mnadhimu, Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Solomon Urio anayetoka Makao Makuu
kwenda Magereza Mkoa wa Dar es Salaam kuwa Afisa Mnadhimu pamoja na aliyekuwa
Boharia Mkuu wa Jeshi la Magereza Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza SACP
George Kiria amehamishiwa Makao Makuu Kitengo cha Uhasibu .
Mabadiliko hayo ni ya kawaida na yanalenga kuboresha
utendaji kazi na ufanisi wa Jeshi la Magereza.
Imetolewa na:
Lucas Mboje - ASP
Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza
Makao Makuu ya Magereza Tanzania Bara
07 Januari, 2017.