YUSUF MANJI WA YANGA NAYE AISOMA NAMBA,SERIKALI YA MAGUFULI YAMBANA KISAWASAWA,SOMA HAPO JYHYA
YY
Mfanyabiashara Yusuph Manji jana alitii sheria bila
shuruti kwa kuhama kwenye jengo la Quality Plaza akitekeleza amri ya Mahakama
ya kumtaka kurejesha jengo hilo ambalo ni mali ya Mfuko wa Pensheni kwa
Watumishi wa Umma (PSPF).
Mbali na kutekeleza amri ya kuhama baada ya kupewa
notisi ya saa 24 iliyomalizika juzi, pia anatakiwa kulipa malimbikizo ya deni
la pango la Dola za Marekani 6.1 milioni (zaidi ya Sh13 bilioni), ambazo kama
asipozilipa mali zake zitakamatwa.
Hatua hiyo imekuja baada ya Mahakama Kitengo cha
Ardhi kutoa hukumu ya kumtaka Manji kuondoka kwenye jengo hilo pamoja na
kuilipa deni la pango.
Alipotakiwa kuzungumzia suala hilo, Manji ambaye ni
Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga hakupatikana kupitia simu yake ya mkononi.
Viongozi wa kampuni za Manji waliokuwa wakisimamia
uondoaji wa vifaa uliomalizika jana asubuhi, walikataa kuzungumza na waandishi
wa habari waliofika kufuatilia tukio hilo.
Tangu juzi chini ya usimamizi wa kampuni ya udalali
ya Yono Auction Mart, Manji na kampuni zake walikuwa wanaondoa vifaa mbalimbali
vilivyopo kwenye jengo hilo na kuhitimisha shughuli hiyo jana.
Meneja Uendeshaji wa Yono Auction Mart, Atukuzwe
Mhugo alisema kampuni ambazo walikuwa wakizisimamia kuondoa vifaa ni Quality
Group Co Ltd, Gaming Managemeti Ltd, Q Consult Ltd na Quality Logistics Co Ltd.
Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo ya
Yono, Scholastica Kenyela alisema tayari wameshaziondoa kampuni za Manji kwenye
jengo hilo.
Kenyela alisema mteja wao ambaye ni PSPF alichukua
uamuzi huo baada ya Manji kushindwa kulipa kodi ya pango ya zaidi ya Sh13
bilioni.
“Sisi tumetimiza wajibu wetu, ukienda
pale utaona tayari tumeshafanya kazi yetu kwa sababu alipewa notisi ya saa 24
awe ameondoka,” alisema.
Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi
alisema masuala yote yanayohusiana na jengo hilo kwa sasa yako chini ya Yono
Auction Mart. “Sipo Dar es Salaam na sitazung- umzia chochote kuhusu jengo
hilo wenye mamlaka ni Yono naomba uwatafute wao,” alisema.