SERIKALI YASEMA MAPAMBANO YA RUSHWA YAMEIMARIKA,SOMA HAPO KUJUA
Katika jitihada zake za kulinda, kukuza Maadili na
haki za binadamu na kuhakikisha maadili na pambambano dhidi ya Rushwa
yanaimarika, serikali imesema hadi sasa imeshaingiza baadhi ya
mikataba ya kimataifa na kikanda katika sheria za nchi pamoja na kuboresha
sheria zilizopo ili kila mwananchi aweze kupata haki yake
Waziri wa Katiba na Sheria Harrison Mwakyembe
ameyasema hayo leo Jijini
Dar es Salaam kwenye Uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya kutoa huduma na kupokea
kero kutoka kwa wananchi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya
maadili kitaifa na haki za binadamu ambayo yatakayofanyika 10 december
10, mwaka huu
Mwakyembe ameeleza kuwa, Serikali itaendelea
kuhakikisha malalamiko ya kila mwananchi yataheshimiwa na kutatuliwa kwa wakati
na endapo atatokea mtumishi yoyote wa umma akatenda kinyume na
maadili ya kazi hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Akimkaribisha waziri wa Katiba na sheria, Waziri wan
chi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora
Angella Kairuki amebainisha kuwa tangu uhuru upatikane, Nchi ya Tanzania
imekuwa ikisimamia misingi ya maadili haki za binadamu , utawala bora na
mapambano dhidi ya rushwa ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na
kuwa na maendeleo endelevu.