Zinazobamba

WITIKIO NI MKUBWA SANA WA WANANCHI KUELEKEA WAKILI MARATHON-ADDO.

Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania (TPBA) Addo November,amesema idadi imezidi kuwa Kubwa sana ya Wananchi ambao wanaendelea kujitokeza Kwa Wingi kutoka pande Mbalimbali za Nchi Kwaajili ya kujisajili Kuelekea Wakili Marathon.

Addo ameyasema hayo Leo Mei 15,2026, Katika Ukumbi wa TFF Wilaya ya Ilala Jijini Dare s salaam, Wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuelekea Wakili marathoni ambayo Inatarajiwa kufanyika Mei 31,2026 Jijini Dodoma.

Addo amesema,Ada ya Usajili ni shilingi elfu 40,000 ambapo Mshiriki atapatiwa marathon Kit yenye T-shirt, Bib No. String bag (kibegi) na Medal (baada ya kukimbia) Na atakayelipa 1,50000 atapata Marathon Kit pamoja na Tracksuit.“Sisi Mawakili wa Serikali tunafanya kazi nyingi za kisheria katika kusaidia nchi yetu kwa kushirikiana na mawakili binafsi, hivyo tunaungana pamoja kwenye marathoni hii ambapo tutaweka miili yetu sawa kwa kushiriki mbio fupi na ndefu pamoja na watoto. Wananchi nawakaribisha sana waendelee kujisajili,” amesema Wakili Addo.

Vilevile addo amesema marathoni hiyo itahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kiserikali akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe, Hamza Johari, huku akieleza kuwa jiji la Dodoma linatarajiwa kufurika kutokana na idadi kubwa ya washiriki ambao wanaendelea Kuitikia wito huo wa Kushiriki Wakili Marathon.

Sambamba na hayo, Wakili Addo amesema kupitia mbio hizo wataendelea kuhamasisha utoaji wa msaada wa kisheria kwa wananchi, akibainisha kuwa Mawakili wa Serikali walishiriki kikamilifu katika kampeni ya Mama Samia Legal Aid Campaign iliyowafikia zaidi ya wananchi milioni nne nchini kote.“Katika kampeni ya Mama Samia Legal Aid tuligundua kesi zinazowasumbua wananchi kwa kiwango kikubwa ni migogoro ya ndoa na ardhi,” amesema addo.

Katika Marathon hii pia,Bingwa wa dunia wa mbio ndefu, Alphonce Felix Simbu, anatarajiwa kushiriki Marathoni ya Mawakili wa Kiserikali inayotarajiwa kufanyika Mei 31, 2026 jijini Dodoma, ikiwa na lengo la kuhamasisha wananchi kutambua haki zao pamoja na kupata msaada wa kisheria.Naye mwanariadha wa zamani wa mbio za marathoni nchini, Juma Ikangaa, amewahamasisha wanawake kujitokeza Kwa Wingi kushiriki marathoni hiyo, akisema wanawake wana uwezo mkubwa wa kufanya vizuri katika mashindano ya riadha.

Vilevile Ikangaa amesema,Marathon Hizi zitaibua kina simbu wengi Kwasababu marathon Hizi zitaenda kuibua vijpaji vingi sana Nchini.

Ikangaa amesema historia inaonyesha kuwa hata mwaka 1965 mwanamke mmoja aliwahi kushinda medali katika mashindano ya riadha, hivyo hakuna sababu ya wanawake kujiweka nyuma  nyuma katika mashindano haya.



No comments