BREAKING NEWS,RAIS MAGUFULI AWARUHUSU WAMACHINGA KUFANYA BIASHARA,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
WAKATI Wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya nchini
wakiwachachamalia wafanyabiashara wadogodogo (Wamachinga) wakiwataka watoke
maeneo mbali mbali wanayofanyiaa biashara kwa madai wanafayanyia maeneo yasiyo
rasmi huku wakiwataka waende kwenye maneno husika yaliotengwa.
Hatua hiyo, imemuibua Rais John Magufuli baada
ya kuwataka viongozi hao wa mkoa na Wilaya waache
kuwabaguzi wafabiashara hao,kwa madai hilo ni kundi muhimu linahitajika kupewa nafasi katika nchi.
Hata hivyo,Rais Magufuli ameelekeza Wafanyabiashara hao wasiondolewe mahali
walipo bila ya kuwekewa mazingira mazuri na rafiki ya biashara huko waendapo.
Akizungumza na Waandishi wa habari kwa niaba ya Rais
Magufuli,Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa
(Tamisemi) George Simbachawene amesema Rais Magufuli licha ya kuwapongeza wakuu
wa mikoa na wilaya kwa kazi nzuri ila ameonyesha masikitiko yake kwa hatua inayochukuliwa kwa wamachinga nchini .
Amesema Rais amewataka viongozi na watendaji hao
kuangalia ufumbuzi utaratibu mzuri wa
kuwashirikisha wajasiliali hao ili kupata ufumbuzi ulioshirikishi kuriko utaratibu wa sasa wakuwafukuza
wafanyabishara hao.
“Kwa kuanzia ni vyema yakatengwa maeneo ya katikati ya
mji yenye wateja wa bidhaa zinazouzwa kwa kuangalia uwezekano wa kufunga mtaa japo
mmoja ili utumike kwa kazi za kimachinga”amesema
Waziri Simbachawene.
Waziri Simbachawene amefanunua kuwa utaratibu huo
hautamaanisha kwamba watu wapange bidhaa
zao Barabarani bali wanatakiwa kupanga
bidhaa hizo kwenye maneno maalum ambayo yanatengwa.
Hata hivyo,Waziri huyo amesema Rais amezitaka Mamlaka husika zinatakiwa ziandae maeneo
Rafiki yenye mahitaji muhimu kwa wafanyabishara hao ili yawezee kufikika kiraisi kwa
wafanyabiashara hao.