TRA YAWAPIGA MSASA MADALALI WA BIMA NCHINI,SOMA HAPO KUJUA
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa mafunzo ya
siku moja kwa Madalali wa Bima Tanzania yenye lengo la kuwajengea uwezo wa
kuifahamu vema Sheria ya Kodi ya Mwaka 2014 ili waweze kushiriki vema na
kuondoa kasoro katika ulipaji wa Kodi ya ongezeko la Thamani kutoka Sekta ya
Bima.
Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Elimu kwa Mlipa
Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Diana Masalla wakati wa mkutano
waandishi wa habri kwenye semina ya siku moja kwa Madalali wa Bima( Insurance
Brokers) ya kuwajengea uwezo kuhusu Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).
Amesema kuwa mafunzo hayo yamewaelimisha wanachama
hao juu ya Kodi ya zuio , utoaji wa kodi ya ongezeko la Thamani (VAT) na jinsi
ya kulipa kwa njia ya mtandao(Revenue gateway system). Ameongeza kuwa TRA
imekuwa ikitoa mafunzo hayo kwa Wanachama na Mawakala wa Bima kwa sababu kabla
ya Sheria ya Mwaka 2014 walikuwa halipi Kodi na hivyo semina hiyo imesaidia
wanachama hao kuwa na uelewa mpana juu ya ulipajji wa kodi ya ongezeko la
thamani.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama cha Madalali wa
Bima Tanzania Mohamed Jaffer aliipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa
hatua yake ya kutoa elimu kwa wanachama wake kwani imesaidia sana kuwajengea
uwezo ambao utasaidia ulipaji wa Kodi ya Ongezeko la Thamani.
Jaffer ameongeza kuwa ni muhimu sana wanachama wa
Chama chake kuelewa vema jinsi ya kujaza na kulipa kodi kwani asilimia 60 ya
mapato ya Bima yanatokana na madalali wa Bima kwa kuwa wao ndio wako karibu na
wateja kuliko Kampuni za Bima ambazo zinabaki na asilimia 40.
Kati ya fedha hizo asilimia 18 ndio ulipwa kodi ya
ongezeko la thamani na kuongeza kuwa kiwango cha makusanyo kwa mwaka huu
kinatarajjiwa kuongeza na hivyo kuongeza mapato ya kodi ya VAT.