SAKATA LA KUPOTEA KIGOGO WA CHADEMA,JESHI LA POLISI WAIBUKA,SOMA HAPO KUJUA
Ukiwa umetimia mwezi mmoja, baada ya Msaidizi wa
Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Benard Saanane kupotea, Jeshi la Polisi limesema linachunguza taarifa za
kupotea kwake ambazo ilizopokea kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kama rafiki wa
Saanane Desemba, 5, 2016.
Wakati akizungumza na waandishi wa habari, Desemba
21, 2016 Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, CP Robert Boaz
amesema Jeshi la polisi limefungua jalada la uchunguzi na kwamba taratibu za
kiupelelezi za mtu aliyepotea zilifuatwa na bado upelelezi wa suala hilo
unaendelea.
“Tuanashukuru wananchi wanaotupatia
taarifa kuhusu tukio hilo, tunaahidi kwamba taarifa hizo tutazifanyia kazi.
Tunazidi kuwaomba wananchi wenye taarifa za kupotea Saanane waziwasilishe
katika kituo chochote cha polisi,” amesema.
Sambamba na hilo, Kamishna Boaz amefafanua tukio la
uzikwaji wa maiti saba zilizokufa maji katika mto Ruvu, pasipo kufanyiwa
uchunguzi wa kutambua waliokufa na chanzo cha vifo vyao.
“Mtakumbuka kati ya tarehe 6 hadi 12,
1016 huko mto Ruvu jeshi la polisi lilipata taarifa ya kuonekana maiti saba
zikiwa zinaelea mtoni kwa nyakati na maeneo mbalimbali, baada ya taarifa hizo
kupatikana askari na daktari walifika eneo la tukio na kufanya uchunguzi wa
kitaalamu,” amesema na kuongeza.
“Kutokana na ukweli kwamba baadhi ya
maiti zilikuwa zimeharibika, maiti 6 ziliamuliwa kuzikwa katika eneo la tukio
na moja yenye unafuu ilipelekwa hospitali ya wilaya ya Bagamoyo kwenye chumba
cha maiti hadi pale ilipozikwa na halmashauri baada ya maiti hiyo kutotambuliwa
na mtu yeyote.”
CP Boaz amesema hatua zote za kitaalam zilifuatwa na
kwamba upelelezi unaendelea kufanywa ikiwemo wa kuwatambua marehemu hao na kujua
chanzo cha vifo vyao