RC MKONDA AMUAPISHA MKUU WA ILAYA YA UBUNGO,SOMA HAPO KUJUA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda
amemuapisha Kisari Matiku Makori kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kufuatia uteuzi
uliofanywa na Rais Magufuli kwa Wakuu wa Wilaya hivi karibuni.
Akimuapisha Mkuu huyo wa Wilaya RC Makonda ameeleza
kuwa wananchi wa Ubungo wanamatumaini na uteuzi wake na lengo kuu la kuanzisha
wilaya ya Ubungo ni kusogeza huduma za wananchi karibu hivyo inabidi ahakikishe
anatatua changamoto zao kwa kuwafuata huko waliko na asiridhike na ripoti anazoletewa
ofisini kwani kumekuwepo na changamoto kubwa ya uwajibikaji hivyo inabidi
hajiridhishe kwanza.
Katika hatua nyingine RC Makonda amewaagiza wakuu wa
wilaya wote kutoruhusu wananchi kubomolewa nyumba zao mpaka kuwepo hukumu
halali ya mahakama kwani wananchi wamekuwa wanaonewa na kudhulumiwa haki zao,
hivyo wakuu wa wilaya kwa kushirikiana na jeshi la polisi wahakikishe haki
inatendeka kwa kufuatilia ukweli na kujiridhisha kwa kuzikagua nyaraka husika.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya huyo Makori ameomba ushirikiano
kwa viongozi wenzake ili aweze kutimiza majukumu yake kikamilifu na kuahidi
kuwa atafanya siasa za kuleta maendeleo ili kila mwananchi anufaike na
rasilimali zilizopo.