TUNDU LISSU AKAMATWA NA KUACHIWA NA POLISI KISA KUMWITA RAIS MAGUFULI "MTUKUFU"SOMA HAPO KUJUA
Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chadema (katikati)
akizungumza na vyombo vya habari muda mchache baada ya kutoka kuhojiwa na
polisi
|
TUNDU
Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), ameachiwa baada ya kukamatwa na kuhojiwa Jeshi la Polisi katika
Kituo Kikuu cha Kanda Maalum ya Dar es Salaam, anaandika Faki Sosi.
Mapema leo asubuhi
Lissu alikamatwa na kupelekwa kituoni hapo ambapo ilielezwa kuwa alichukuliwa
kwa lengo la kuhojiwa kuhusiana na mkutano aliofanya na waandishi wa habari
kuhusu wa kupotea kwa Bernard Saanane.
Ben
Saanane alikuwa Msaidizi wa Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chadema Taifa –
alipotea ghafla takribani mwezi mmoja sasa na hajulikani alipo huku Lissu
akiitisha mkutano na wanahabari tarehe 14 Desemba, 2016 na kuitaka serikali
ieleza kama inamshikilia kijana huo au la.
Fredrick
Kihweru mmoja kati ya wanasheria wa Chadema akitoa maelezo baada ya mahojiano
ya polisi na Lissu kumalizika amesema, “aliitwa kuhojiwa juu ya Press
conference aliyofanya na kuzungumzia suala la Saanane lakini pia wamemuhoji
anamaanisha nini kumwita Rais John Magufuli jina la “Mtukufu.”
Itakumbukwa
kuwa Lissu amekuwa akimtaja Rais Magufuli kama “mtukufu” mara kadhaa tangu
aliposhitakiwa kwa kutamka kuwa “Dikteta uchwara anapaswa kupingwa kwa nguvu
zote” kesi ambayo bado inaendelea mahakamani.
Wakili
Kihweru amesema Lissu amehojiwa pia kuhusu hatua yake ya kuitaka Serikali iseme
kama haimshikilii Ben Saanane na pia ieleze juu ya mawasiliano yake ya mwisho
ya Ben alifanya na nani, wapi na waliwasiliana nini.
Baada
ya mahojiano hayo Lissu ameachiwa kwa dhamana na anaweza kuitwa wakati mwingine
atakapohitajika.