Zinazobamba

BAA YA KWETU PAZURI TABATA YAFUNGWA,SOMA HAPO KUJUA




Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto ameagiza kufungwa kwa ukumbi maarufu wa Starehe ujulikanao kwa jina la Kwetu Pazuri Tabata kutokana na kushindwa kukidhi vigezo.

Akizungumza na Globu ya jamii mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku mbili ,Kumbi la Moto amesema kuwa wameamua kufunga ukumbi huo mara baada ya kufanya na ukaguzi na kujiridhisha kuwa haijakidhi vigezo.
"Tumefanya ukaguzi na kumchukua Meneja wa Bar hiyo na kumfikisha kituo cha Polisi Ukonga Stakishari kwa ajili ya kufunguliwa mashataka na baadae kufikishwa mahakamani"amesema Kumbilamoto.

Amesema kuwa mara baada ya kutoka katika kituo hicho ,alifikishwa kituo cha Polisi kati na kukubali kulipa faini ya Milioni mbili na kukukiri makosa ya kufanya kazi ya Night Club bila kuwa na leseni huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Aidha tumewaonya juu ya tabia yao ya kupanga viti karibu na barabara jambo ambalo ni kinyume cha sheria za Tanroads, " hivyo  tumeamua tuifunge mpaka hapo watakapo jipanga upya",Kumbi la Moto amesema na kuongeza kuwa kwa muda mrefu watu walikuwa wakilalamika juu ya sehemu hiyo lakini hatua zilikuwa zinachelewa kuchukuliwa, hivyo nimefika katika eneo la tukio na kujionea hali halisi na kuamua kuifunga Bar hiyo.




Aidha katika ziara hiyo pia amekagua ujenzi wa maabara ya Zahanati ya kata ya vingunguti ambayo inatarajia kukamilika hivi karibuni.