MEYA DAR ES SALAAM AWAONYA WAKUSANYA USHURU WA MAEGESHO
Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akifafanua jambo kwa wandishi wa habari leo kuhusiana na suala zima la tozo za maegesho ya magari
MEYA wa Jiji la Dar es Salaam,
Isaya Mwita amewataka wakandarasi hususani wanaokusanya ushuru wa maegesho, waanze
kutumia mashine za EFDs walizokabidhiwa vinginevyo mikataba yao iko hatarini
kusitishwa.
Akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake, Meya Mwita amesema kwa muda mrefu wakandarasi hao
walikuwa wakitumia mashine za mkono, wamebaini mapato mengi yalikuwa yakipotelea
mifukoni mwa watu wachache na sasa ni agizo kwa wazabuni wote wa wilaya za
Daresalaam kutumia mashine za Kielectroni.
Amesema kupitia mashine hizo
wanahakika mapato yataongezeka kutoka shilingi milioni 170 iliyokuwa
inakusanywa hapo awali kwa mwezi hadi kufikia Zaidi ya Shilingi Milioni 370 kwa
mwezi.
Katika hatua Nyingine, Isaya
Mwita amewaonya wakandarasi hao kuangalia namna ya kuwadhibiti wafanyakazi wao
kwani hivi sasa wamezusha tabia ya kuwanyanyasa wakazi wa Jiji la Darsalaam
kinyume cha makubaliano ya mkaba.
Amesema kumekuwa
na tabia za wakandarasi isivyo halali wakazi wa jiji wanaoegesha magari yao,pamoja
na kutumia lugha za matusi kwa kisingizio cha kufuata sheria za Jiji.
Amesema
sheria ya Jiji hairuhusu matumizi ya mabavu, matusi, kejeli kwa watu
wanaoegesha gari zao, wanachopaswa kufanya ni kufuata sharia ambazo
wamekubaliana katika mikataba yao ya kazi.
Meya
ameyataja majukumu ya kimkataba ambayo wakandarasi wote wanapaswa kufuata ni
kama ifuatavyo,:
1
.Wakala atafanya kazi hii bila Kuvizia magari ya wananchi kwa lengo la
kujipatia pesa .
2.
Wakala atafanya kazi hii kwa weledi mkubwa kwa kuzingatia Sheria, Miongozi,
Maelekezo, Kanuni na taratibu zilizopangiwa pasipo kusababisha bughuza ,kero na
usumbufu kwa Wananchi.
3.
Wakala anatakiwa kutoa muda wa dakika sitini [60] kabla ya kuchukua mamuzi ya
vuta gari, Bodaboda au bajaji lililovunja sheria, kuzuia . Lakini kwa
gari , Bajaji au Bodaboda iliyozuia barabara itaondolewa mara moja ili kuondoa
msongamano.
4.Wakala
anapaswa kuepuka kutoa Lugha ya Matusi au udhalilishaji .
4.Wakala
anapaswa kuruhusu gari ,Pikipiki au Bajaji kuegeshwa kwa dharura sehemu
isiyoruhusiwa kwa muda usiozidi dakika Thelasini [30] kama Dereva ameweka
viashiria vya tahadhari. Isipokuwa kwa wale wenye magari yenye hitilafu inaweza
kuzidi mpaka saa moja [yaani dakika 60] baada ya kujirizisha na dharura
iliyojitokeza.
5.
Wafanyakazi wanapaswa kuwa na sare pamoja na vitambulisho vya kazi .
6.
Wakala anatakiwa kutoa faini zilizoainishwa na jiji na sio vinginevyo.
7.
Wakala anapaswa kutumia risiti za mashine za Kielekronikia.
8.Magari
yanayotumika katika utekelezaji wa kazi hii yanatakiwa yawe na Stika kubwa
inayoonyesha jina la kampuni pamoja na namba ya simu ya wakala.
9.Wakala
anatakiwa kutumia risiti [Point of Sale, [POS] za Halmashauri ya jiji.
10.
Wakala anatatakiwa kutoa taarifa ya utekelezaji wa kazi hii kwa MWAJIRI Kila
baada ya Wiki Mbili.
11.Wakala
anatakiwa kufanya kazi katika maeneo aliyoelekezwa na MWAJIRI nasio vinginevyo.
12.
Wakala anapaswa kushirikiana na jeshi la polisi pamoja na Mamlaka zingine pale
inapohitajika katika utekelezaji wa kazi husika.
Sasa
anashangazwa kuona mikataba hiyo inavunjwa, amesema hatosita kufuta zabuni zote
kwa kitendo cha kukiuka makubaliano hayo.