Zinazobamba

AFYA YA MBUNGE LEMA YAWA GOIGOI,ASHINDWA KUTINGA MAHAKAMANI,SOMA HAPO KUJUA




Kesi iliyokuwa isikilizwe leo 22 disemba 2016 inayomkabili mbunge wa Arusha mjini Godbless Leman na mkewe Neema Lema ya kumtukana mkuu wa mkoa Mrisho Gambo imeahirishwa kutokana na hali ya lema kuwa mbaya gerezani.

Taarifa za Lema kushindwa kufika mahakamani zimetolewa na wakili wa serikali Elizabeth Swai leo asubuhi kwa hakimu mfawidhi katika mahakama ya hakimu mkazi Augustino
Rwezile ,alisema alipata taarifa kutoka kwa Afisa Magereza mshatakiwakwanza anumwa hivyo siku ya leo alipewa mapumziko pamoja na hayotaarifa hizo hazijaeleza kwa  undani ni tatizo gani linamsumbua mbunge
huyo.

Pia alisema alipewa cheti cha mgonjwa cha zahanati
ambacho kilionyesha mahudhurio ya mgonjwa kwenye zahanati hiyo kutokana na kuwepo na taarifa za kuumwa za mbunge huyo na kushindwa kufika mahakamani,aliiomba mahakama ipange tarehe nyingine .

Leo ilikuwa ni siku ya kusomewa hoja za awali kwa mbunge huyo na mkewe Neema Lema , ambapo pia shahidi wa kwanza kutoka jamhuri alikuwa Georgr Katabazi alikuwa anatoa ushahidi.
Hata hivyo hakimu mfawidhi Augustino Rwezile amesema kuwa kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 18 Januari 2017

Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema na mkewe Neema Lema wanakabiliwa na kesi ya mkumtukana mkuu wa mkoa Mrisho Gambo.