MAZISHI YA KIHISTORI IRINGA MAREHEMU AZIKWA KABURI MOJA NA KONDOO
Wanafamilia wakiwa wamelizungika kaburi la marehemu Ngaga aliyezikwa kaburi moja na kondoo pamoja na kuku mweusi leo kwenye kitongoji cha Mkawaganga kijiji cha Mbigili wilaya ya Kilolo mkoani Iringa
Mganga wa kienyeji Galasiano Nyenza (kulia) akiwa na mtoto wa marehemu Andrea Ngaga ,Kurugenzi Ngaga kushoto baada ya kufanyika kwa mazishi ya kimila katika kijiji cha Mbigili Kilolo kwa marehemu kuzikwa kaburi moja na kondoo na kuku mweusi
Mganga Nyenza aliyeongoza mazishi hayo katikati akiwa na baadhi ya ndugu kando ya kaburi
Waombolezaji wakitoka kuzika
Marehemu enzi za uhai wake
Nyumbani kwa marehemu waombolezaji wakiwa kwenye foleni
....................................................................................................
Na MatukiodaimaBlog
MAMIA
ya wakazi wa kijiji cha Mbigili na mji wa Ilula katika wilaya
ya Kilolo wamefurika katika mazishi ya aina yake yaliyofanyika
katika kitongoji cha Mkawaganga kijiji cha Mbigili wilaya ya kilolo
mkoani Iringa kushuhudia mazishi hayo ya kihistoria baada ya mzee
mmoja aliyefariki dunia ghafla kuzikwa kaburi moja na kondoo pamoja na kuku
mweusi.
Tukio
hilo limetokea leo wakati wa mazishi ya mzee Andrea Ngaga (90)
mkazi wa kitongoji cha Mkawaganga aliyekuwa akijishughulisha na kazi
za uganga wa kienyeji kijijini hapo enzi za uhai wake .
Baadhi
ya wananchi waliofika katika mazishi hayo walisema kuwa
walilazimika kusitisha shughuli zao za shamba na biashara na
kufika kushuhudia mazishi hayo ambayo ni mara ya kwanza kufanyika
katika kijiji hicho alisema John Mfaligoha kuwa kabla ya kifo
marehemu huyo alipata kuwaeleza aina ya mazishi yake yatakavyokuwa .
Hivyo
alisema wananchi waliowengi walifika kutaka kushuhudia tukio
hilo la mazishi na ndio sababu iliyopelekea wananchi kusukumana
msibani wakati wa mazishi kwa kila mmoja kutaka kushuhudia tukio
hilo la kihistoria katika kijiji hicho.
Mwenyekiti
wa serikali ya kijiji cha Mbigili Ibrahim Rashid (46) alisema
amezaliwa katika kijiji hicho tukio hilo ni la kwanza kufanyika
hajapata kushuhudia mazishi ya aina hiyo zaidi ya kusikia katika
vyombo vya habari kutoka nje ya kijiji chake na kuwa mazishi hayo
yamefanyika kimila zaidi na kimsingi huwa marehemu anachagua mtu wa
kuzikwa nae kabla ya kifo .
Ila
hakuweza kuacha maagizo zaidi ya kuomba pindi atakapokufa kuzikwa
kimila na ndio sababu aliyeongoza mazishi hayo ni mganga wa
kienyeji kutoka Ifunda wilaya ya Iringa Galasiano Mfaume Nyeza
ambae ni baba mdogo na marehemu huyo .
Mtendaji
wa serikali ya kijij hicho cha Mbigili Thabith Kalolo alisema kuwa
kimsingi hakuna kosa lolote familia ambalo wamelifanya kwa
kufanya mazishi ya aina hiyo kwani serikali haiingilii uhuru wa
wananchi wake kuamini masuala ya mila na kuwa iwapo mazishi hayo
yangekiuka haki za binadamu mwingine mfano kama wangekata kumzika
marehemu na binadamu mwingine aliyehai hapa isingewezekana ila kwa
kumzika na kondoo na kuku mweusi hakuna shida .
Hata
hivyo alisema tofauti ya rekodi ya misiba iliyopata kutokea
katika kijiji hicho ,msiba wa mganga huyo umevunja rekodi kwa
kuhudhuriwa na idadi kubwa ya watu na kuwa msiba uliovunja rekodi
kwa michango ni huo pekee kwani misiba mingine fedha za rambi rambi
huwa ni kati ya Tsh 300000 hadi 500000 mwisho ila msiba huo rambi
rambi ni zaidi ya Tsh milioni 1.3
Mtoto
wa marehemu Kurugenzi Ngaga alisema kuwa babake alifariki dunia
juzi Desemba 20 majira ya saa 6 usiku mwakla huu kuwa alikuwa
akisumbuliwa na tatizo ya chembe ya Moyo na kuwa ameacha wajane
wawili na watoto 19.
Kurugenzi
alisema kimila kama ingekuwa zamani marehemu angezikwa na mjukuu
wake aliyemteua kushika mikoba yake ila kutokana na mambo ya mila
kwa sasa kupewa kisogo waliona ni vema wakamzika na kondoo na kuku
huyu mweusi .
...........Usikose Mwendelezo wa Habari hii ...........................................