MBUNGE LEMA AENDELEA KUTESEKA,MAHAKAMA YAMNYIMA DHAMANA LEO,SOMA HAPO KUJUA
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imemnyima dhamana
Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) Godbless Lema. Mahakama hiyo imeeleza kuwa
mawakili wamtuhumiwa huyo walipaswa kuonesha kusudio la kukata rufaa ndani ya
siku10 kabla ya kukata rufaa.
Hii ni mara ya tano mbunge huyo anakosa dhamana
mahakamani tangu alipokamatwa Novemba 3 mwaka huu akiwa mjini Dodoma na
kusafirishwa hadi Arusha katika kesi ya uchochezi inayomkabili.
Katika kesi ya msingi lema anatuhumiwa kutoa maneno
ya kichochezi dhidi ya Rais Magufuli kwa madai kuwa Mungu ndiye aliyemwambia
maneno hayo wakati akiwa anaomba.