RAIS MAGUFULI KULILIZA KANISA KATOLIKI NCHINI,AGIZO LAKE KUVIMALIZA VYUO VYA KANISA HILO,SOMA HAPO KUJUA
RAIS
John Magufuli agizo lake la kutaka orodha ya vyuo vikuu nchini iangaliwe upya huku akitoa maelekezo ya kutaka kubakiwa
na vyuo vikuu vichache vyenye sifa,sasa
agizo hilo linatajwa uwenda likaliweka pabaya Kanisa Katoliki nchini ambalo
ndio linatajwa kumiliki vyuo vikuu vingi.(Mtandao huu umeelezwa).Anaandika
KAROLI VINSENT endelea nayo.
Rais
Magufuli mara kwa mara amekuwa akiitaka
Tume vya Vyuo Vikuu nchini (TCU) kuangalia na kupunguza wingi wa vyuo vikuu
nchini kwa kile anachokisema vyuo vikuu vingi vimeanzishwa huku vikiwa havina
sifa ya kuwa vyuo vikuu.
Pamoja
na hayo Rais Magufuli alielekeza TCU kuangalia na kuhakikisha wanabakiza vyuo
vikuu vichache huku akivitaja kwa majina
vyuo vikuu hivyo ni chuo kikuu cha Mliman na chuo kikuu cha Dodoma kwa
kile anachodai kinanafasi ya kuchukua wanafunzi wote wanaohitajika kuingia chuo
kikuu.
Baada
ya Agizo hilo la Rais,linatajwa litaliweka pabaya Kanisa Katoliki kutokana na
kutajwa kumiliki vyuo vikuu vingi sana nchini huku ikitafsiriwa agizo hilo
uwenda likalilenga kanisa hilo.
Kwa
mujibu wa mtoa taarifa wetu aliyoko ndani ya (TCU) ambaye hakutaka kutajwa jina
lake mtandaoni,ameumbia mtandao wa (Fullhabari.blog) kuwa agizo hilo linaligusa
moja kwa moja Kanisa Katoliki nchini ambapo linatajwa kutajwa kumiliki vyuo vikuu vingi.
“Nichokwambia
hili agizo lazima litaleta msuguano mkubwa,yaani kanisa Katoliki haliwezi
kupona kabisa ndugu kwani linautilili wa vyuo vingi sana,hata Magufuli
anavyosema vyuo vya (St nan) vingi vinamilikiwa na Kanisa Katoliki pamoja na
Madhehebu mengine,yaani nakuhakikisha lazima vifungwe tu maana mkubwa kaamua
sisi tufanyaje?”amehoji mtoa taarifa wetu huyo.
Uchunguzi
uliofanywa na Fullhabari.blogs umebaini Kanisa Katoliki linatajwa kumiliki vyuo
vikuu vya Mtakatifu Jordan cha Morogoro,Chuo kikuu cha Mwenge,Chuo kikuu cha
Mtakatifu Augustino,chuo kikuu cha
mtakatifu Joseph,Chuo kikuu cha sayansi cha Mwanza pamoja na kutoa matawi mengi ya Vyuo vikuu kutumia mwavuli wa
Chuo Kikuu cha Mtatifu Augustino,
‘”Yaani
kwa mfano chuo cha Mtatifu Jordan hiki
hakiwezi kupona hata katika kukipandisha hazi kwake kilikuwa na utata,leo chuo
cha Sauti kimekuwa na matawi mengi mengine hayana hata hadhi ya kuwa
matawi,yaani nakuhakikishia,lazima kilio kitakuja tu wewe ngojea”kimesema chanzo
chetu.
Mbali
na Kanisa katoliki pigo hilo linatajwa pia kuyagusa madhehebu mengine ambayo
nayo yanatajwa kuhusika katika kuanzisha utilili wa vyuo vikuu ambavyo hata
kuanzishwa kwa kulikuwa na utata.