AJIRA MPYA ZA WALIMU ZAIPASUA SERIKALI YA JPM,NAIBU WAZIRI WAKE AAMUA KUFUNGUKA UKWELI UWEPO WA AJIRA HIZO,SOMA HAPO KUJUA
Naibu Waziri ofisi ya Nchini,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi)Suleiman Jaffo (kulia)akizungumza na Mwandishi wa Fullhabari.blogs Karoli Vinsent (Kushoto)(Picha na Maktaba) |
KILE kinachoonekana kuwa Ajira za Walimu wapya ni
kama zimeanza kuipasua serikali ya awamu ya Tano,baada ya Viongozi wa wakuu
hususani Mawaziri kushindwa kutaja tarehe ya lini serikali itaanza kuajiri
walimu hao wapya,ambapo sasa Viongozi hao wamefunguka na kusema Rais John Magufuli ndio
mwenye sauti ya mwisho kwenye ajira hizo.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo
Hayo yamebainishwa Jana Jinini Dar es Salaam na Naibu Waziri Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Suleiman Jaffo wakati alipokuwa
anaongea na (Fullhabari.blog) ambapo Waziri huyo alisema kwa sasa suala la
ajira za walimu lipo kwa Rais John Magufuli ndio atakapoamua lini zitatoka.
Kauli hiyo
Jaffo inakuwa mara baada ya Mwandishi wa Mtandao huu alipomtaka ataje tarehe
lini serikali itatangaza ajira hizo,alisema serikali ilitakiwa kuajiri walimu
elfu 35 ambapo amedai zoezi hilo lilisitishwa kutokana kupisha uhakiki wa
watumishi hewa.
“Ni kweli tutaajiri walimu ila kama mlimsikia Rais Magufuli wakati alipokuwa anaongea
na waandishi wa habari,alisema serikali imeanza kuajiri ,na kwa kuanzia
wameanza katika chuo cha Mloganzira,ila nakuhakikisha yeye ndio mwenye Mamlaka
hata katika hizo za ajira za walimu wapya,”alisema Waziri Jaffo.
Waziri Jaffo
alisema serikali inampango wa kuajiri walimu waliomaliza vyuo mwaka jana (2015)
na mwaka huu (2016) huki akibanisha kuwa kwa sasa nchi inauhaba wa walimu wa sayansi na hata katika ajira
hizo eflu 35 wataangaliwa walimu watapewa kipaumbele.
Kauli hiyo
Jaffo inakuja ikiwa ni baada ya Viongozi wa Chama cha Walimu nchi(CWT)
wakiitaka serikali ya Magufuli iseme ukweli kuhusu ukweli wa ajira hizo kama
zipo au hazipo,kwa kile wanachokida kuwa serikali haina fedha za kaujiri walimu hao na imeamua kijificha kwenye kichaka cha "Watumishi hewa".
Akihojiwa na
Gazeti la Tanzania Daima mwanzoni mwa hiki hii,Katibu Mkuu wa (CWT), Ezekiah Oluoch
alisema inasikitisha serikali kutokuwa na jibu kamili za ajira hizo kwa kile
anachokisema zoezi gani la uhakiki lisilo kwisha.
“Wasema Ukweli
kama shida ni fedha hakuna za kuajiri watumishi hao,zoezi la kuhakiki gani
mpaka sahivi,maana shule hazina walimu,ziko shule zinamwalimu mkuu tu ndio
anafundisha peke yake,leo walimu wamehitimu wapo mtaani na serikali inashindwa
kujairi kwa hoja ya watumishi hewa”alisema Oluoch.
Sakata la Ajira mpya za Walimu zilianza kuwa ngumu
pale Rais Magufuli Juni mwaka huu alipotangaza kusitisha ajira mpya zote
serikali kwa madai kuwa serikali inahakiki watumishi hewa,na kuahidi zoezi la
hilo litaisha ndani mwezi mmoja na nusu baada ya hapo ajira hizo zitaanza
kutolewa.
Ambapo sasa miezi takribani mitano imepita baada ya
Zuio hilo la Rais Magufuli kupita na hakuna hata ajira hizo za Walimu huku bado
kukiwa na mahitaji makubwa ya awalimu katika shule za Msingi na Sekondali
nchini,
Na inaleezwa kuwa Takribani ya wahitimu ya uwali wa
mwaka 2015 na wa mwaka huu wakiwa wamemaliza mafunzo hayo,huku ikikadiliwa
walimu hao wanafikia zaidi ya elfu 80.