WAMILIKI WA BLOG TANZANIA KUKUTANA WIKI IJAYO,NMB YADHAMINI MKUTANO HUO
Chama
cha Wamiliki/Waendeshaji mitandao ya kijamii nchini (Tanzania Bloggrs
Network-TBN) mapema leo Disemba, 2 imekabidhiwa cheki maalum ya kiasi
cha Tsh. Milioni 10, fedha zilizotolewa na benki ya NMB kama wadhamini
wakuu wa Mkusanyiko wa ‘Bloggers’ kutoka maeneo mbalimbali ya mikoa ya
Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.
Katika
tukio hilo, Mwenyekiti wa muda wa TBN, Bwana Joachim Mushi amepongeza
benki ya NMB kwa kuweza kudhamini tukio hilo muhimu na la kihistoria
kwani litasaidia wana blogger kwa ujumla kuweza kukutana pamoja na
kujifunza kile ambacho wanapaswa kuwahabarisha Umma kupitia blog zao.
“Tunawapongeza
benki ya NMB kwa udhamini huu na tunawaomba sana waendelee kutudhamini
kwani kazi iliyopo mbele yetu kwa sasa ni kutoa elimu sahihi kwa
wenzetu ambao watajumuika katika mkutano huu utakaofanyika siku mbili
yaani 5 na 6 Desemba,2016. Kwa washiriki takribani 150 kutoka Tanzania
nzima ambapo pia tukio hilo litafuatiwa na mkutano mkuu kwa wanachama
hai wa TBN na kujadili mambo mbalimbali,” alieleza Joachim Mushi.
Ofisa
Uhusiano wa NMB, Doris Kilale amesema kuwa wataendelea kushirikiana na
Tanzania Bloggers Network-TBN kwani inaamini kufanya hivyo ni moja ya
njia ya kufikisha ujumbe kwa jamii hasa kupitia mitandao ya kijamii.
“NMB
imekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na wadau wa habari
mbalimbali na sasa tunashirikiana na TBN na tumeweza kutoa kiasi cha
Shilingi milioni 10 kwa ajili ya mkutano wao wa mwaka utakaofanyika 5 na
6 Desemba mwaka huuna. Pia kama munavyofahamu kuwa NMB ipo karibu yako
hivyo kupitia mitandao ya kijamii na Blog itaendelea kufikisha habari
zetu kwa jamii kwa wigo mpana zaidi.” alieleza Ofisa Uhusiano huyo, Doris Kilale.
Mkutano
huo unatarajia kufanyika jijini Dar es Salaam hiyo 5 na 6 Desemba
katika ukumbi wa wa mikutano wa makao makuu ya jengo la Golden Jubilee
PSPF.
Aidha,
mbali na Benki ya NMB kuwa wadhamini wakuu katika tukio hilo, pia
wadhamini wengine ni pamoja na NHIF,SBL, PSPF na Coca Cola ambao wote
kwa pamoja wamejitokeza kufanikisha katika tukio hilo.