TUNDU LISSU AAPA KUPAMBANA NA MAGUFULI MPAKA DAMU YAKE YA MWISHO,SOMA HAPO KUJUA
Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amesema kuwa vyama vya upinzani
vimejipanga vizuri kwaajili ya kukabiliana na Rais Dkt. John Magufuli .
Amesema hayo katika Semina iliyowashirikisha
viongozi wa vyama vya upinzani kutoka Mataifa 16 iliyofanyika Makao Makuu
ya Chama hicho Kinondoni Jijini Dar es salaam, amesema wanapambana
kuhakikisha uwanja wa siasa unakuwa sawa lazima wabadili staili ya
kumkabili Rais Magufuli.
Lissu amesema watafanya siasa ikiwa Magufuli
anataka ama hataki, ama wanavunja Sheria ama hawavunji” Akipiga marufuku
shughuli za kisiasa, hatuwezi kwenda kanisani kuomba, hapana lazima kazi ziendelee
katika aina nyingine”amesema Lissu.
Aidha, Lissu ameongeza kuwa katika Uchaguzi uliopita
haukuwa wa haki na huru ambapo mawakala waliokuwa wakihesabu kura
walikamatwa na kupelekwa polisi.
Hata hivyo ameongeza kuwa hali ya kisiasa ilivyo kwa
sasa kiongozi yeyote atakayefanya siasa anaonekana kama mhalifu na hukamatwa na
kupelekwa mahakamani, hivyo hakuna Demokrasia bali kuna udikteta mkubwa.