JAFFO AWATULIZA WALIMU NCHINI,NI KUHUSU MADENI YAO KWA SERIKALI,MKURUGENZI WA ILALA AMWAGIWA SIFA,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI
VINSENT
NAIBU Waziri
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Suleiman
Jaffo amewataka walimu nchini kuwa na uvumilivu kwa serikali ya awamu ya tano
wakati serikali hiyo inapohakiki madeni yote ya walimu.
Huku akisema zoezi hilo litakwisha hivi karibuni na
kuwaahidi walimu wote watalipwa stahiki zao zote wanazoidai serikali.
Hata hivyo,Jaffo amewahidi tena walimu kuwa serikali
ya Rais John Magufuli imezamilia kuwawekea mazingira mazuri walimu wote nchi
nchini baada ya kumalizika kipindi hiki cha mpito anachodai serikali inaweka mazingira mazuri.
Jaffo,ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam
wakati alipokuwa anazidua majengo mapya
ya darasa katika shule ya msingi Kisutu iliyopo Manispaa ya Ilala Jijini
Hapa,ambapo jengo hilo limejengwa kwa msaada wa Kampuni moja ambapo ujenzi wake
umeghalimu milioni 50,huku uzinduzi huo ulihudhuliwa na walimu wakuu wote wa
shule mbali mbali katika wilaya hiyo.
Kiongozi huyo
ametumia nafasi hiyo kuwatoa hofu walimu baada ya kusema kwa sasa serikali
kupitia Wizara ya yake ya Tamisemi,Wizara ya Elimu pamoja na Wizara ya Fedha na
Mipango kwa pamoja wapo katika kuhakiki madeni yote ya walimu kabla hawajaanza
kuwalipa walimu wote nchini.
Amesema zoezi hilo litamalizika huku akiwaidia
walimu kwa sasa serikali itaweka mazingira mauri kwa walimu.
“Nataka niwakikishieni madeni yenu yote ya walimu
yatalipwa kwa wakati,na serikali ya Magufuli imejipanga kuwawekeezi mazingira
mazuri,nawaambie walimu mtakuwa katika mstari mzuri ambao utawafanya hata walimu
waliohama na kwenda kwenye shule za binafsi
watatamani kuja huku serikali na nafasi itakuwa imefungwa,cha msingi kuweni
na subira”amesema Jaffo.
Pamoja na hayo, Jaffo alimpongeza Mkurugenzi wa
Manipsaa ya Ilala ,Palela
Nitu, kwa hatua yake ya kuwapa kipaumbele walimu
katika manipsaa yake.
“Yaani nikizingiangalia nyuso zenu mnafuraha na kazi
yenu walimu,naimania haya ni matunda ya mkurugenzi wenu wa manispaa kwakuwajari
mpaka mmekuwa na furaha hiyo,”ameongeza
kusema Jaffo,
Naye Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ilala Bwana Nitu alimpongeza Waziri Jaffo kwa kazi nzuri
kwa kuhakikisha anakuja kwa wakati katika kazi mbali mbali zinazohusu wizara
yake.
“Yaani
nikisikia wewe (Jaffo) unakuja kwenye manispaa yangu najua huwa unakuja kwa
wakati,na hata ulipokuja wakati wa kuongea na wafanyakazi wa manispaa uliwai
mapema na hata leo umewai,naimani upo makini katika wizara yako”amesema Nitu.
Kauli hiyo ya Jaffo inakuja ikiwa kumeibuka kwa
kelele mbali mbali kutoka kwa walimu nchini wakiwa wanailalamikia serikali kwa
hatua yake ya kushindwa kuwalipa madeni mbali mbali ya walimu ambayo wanaidai
serikali,Madeni hayo ni fedha za rikizo na kupanda madaraja