Wizara ya Afya nchini yapokea msaada wa Ambulance 10 toka Serikali ya Qatar
Awali kabla ya kupokea magari hayo ya kubebea wagonjwa, yaliyokabidhiwa na Mwakilishi wa Serikali ya Qatar hapa nchii, Balozi wa Qatar, Mh. Abdulla Al Suwaid, Waziri Ummy Mwalimu alimwakikishia Balozi huyo kuwa Wizara yake itayatunza magari hayo na yatafanya kazi iliyokusudiwa huku kipaumbele yakipelekwa katika maeneo yenye uhitaji wa haraka.
“Tunashukuru Serikali ya Qatar kwa kuendelea kushirikiana nasi katika hili. Tunawahakikishia magari haya tutayatunza na yataenda kwenye maeneo yote kusudiwa na kipaumbele zaidi ni pamoja kwenda kusaidia Wanawake Wajawazito.
Pia mbali na Wanawake Wajawazito na Watoto magari haya yataenda katika maeneo yenye uangalizi maalum ikiwemo yale yenye kutokea ajali za mara kwa mara.” Alieleza Waziri Ummy Mwalimu.
Aidha, Magari hayo yanatrajiwa kwenda katika maeneo mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Morogoro, Tanga, Tabora, Kagera pamoja na maeneo ya mikoa ya Kanda ya Ziwa ambapo wameona kuna umuhimu zaidi. Pia kwa Dar es Salaam magari hayo mengine yatapelekwa Wilaya ya Kigamboni na lingine katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ambapo yatasaidia kusafirisha wagonjwa kutoka Hospitalini hapo kwenda uwanja wa ndege kwa ajili ya safari za matibabu.
Kwa upande wake Balozi wa Qatar amebainisha kuwa, Serikali ya nchi yake itaendelea kushirikiana a Tanzania katika kuimalisha mambo mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya.
Wizara ya
Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto. Mh. Ummy Mwalimu
akielezea jambo mbele ya waandishi wa Habari (Hawapo pichani) wakati wa
tukio hilo. kushoto kwake ni Balozi wa Qatar nchini Mh. Abdulla Al
Suwaid
Balozi wa
Qatar nchini Mh. Abdulla Al Suwaid akisoma taarifa fupi wakati wa
kukabidhi magari hayo kwa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia
Wazee na Watoto iliyowakilishwa na Mh. Ummy Mwalimu.
Balozi wa
Qatar nchini Mh. Abdulla Al Suwaid akimkabidhi moja ya funguo ya gari la
wagonjwa (Ambulance) Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na
Watoto. Mh. Ummy Mwalimu
Waziri wa
Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto. Mh. Ummy Mwalimu
akimkabidhi funguo mmoja wa wawakilishi ambapo magari hayo yatapelekwa
Waziri wa
Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto. Mh. Ummy Mwalimu
akifunguliwa mlango wa moja ya Ambulance zilizokabidhiwa kutoka Serikali
ya Qatar
Baadhi ya
wawakilishi ambapo magari hayo yatapelekwa wakiwa na wakionyesha juu
funguo za Ambulance baada ya kukabidhiwa na Waziri ummy Mwalimu.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto. Mh. Ummy Mwalimu akikabidhi funguo hizo
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto. Mh. Ummy Mwalimu akikabidhi funguo hizo
Waziri wa
Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto. Mh. Ummy Mwalimu
akipokea funguo 10 za Ambulance baada ya kukabidhiwa kutoka kwa Balozi
wa Qatar
Waziri wa
Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto. Mh. Ummy Mwalimu
akikagua maeneo ya ndani ya Ambulance hiyo mara baada ya kukabidhiwa.
Waziri wa
Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto. Mh. Ummy Mwalimu akiwa
ndani ya upande wa dereva baada ya kukabidhiwa.
Moja ya Ambulance zilizokabidhiwa na Serikali ya Qatar
Waziri wa
Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto. Mh. Ummy Mwalimu
akikabidhi funguo kwa moja ya wawakilishi wa mikoa ambao gari hizo
zitakazo kabidhiwa.
Waziri wa
Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto. Mh. Ummy Mwalimu akiwa
na Balozi wa Qatar nchini Mh. Abdulla Al Suwaid mara baada ya
kukabidhiwa magari hayo.