Zinazobamba

CUF YAMTAJA MGOMBEA WAKE UBUNGE JIMBO LA DIMANI,SOMA HAPO KUJUA


Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage (kushoto) akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ofisini kwake jijini Dar es salaam  leo mara tu baada ya kuapishwa Ikulu.


 

Chama cha Wananchi Cuf kimethibitisha kushiriki uchaguzi mdogo ujao wa jimbo la Dimani visiwani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mwenyekiti wa tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Semistocles Kaijage, amesema kuwa chama hicho kitawakilishwa na mgombea wake Abdulrazak Khatibu Ramadhani katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Dimani.


“Wagombea wengine ni Hamadi Mussa, ACT Wazalendo, Abdala Kombo khamis, chauma.Abdulazak Khatibu cuf Peter A. Magwira DP, Ali khamis Abdalla NRA. Sau Amour haji ali,SAU. TLP Pandu Haji Punda, UMD,Abdullsamad Salum Ali, UPDP,Bakari Omar.


Sambamba na hayo kaijage amesema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 31(1) b cha sheria ya Taifa ya uchaguzi sura ya 343 na kifungu cha 41( 1) vya sheria ya uchaguzi ya serikali yamitaa sura ya 292, tume imefanya uteuzi kwa wagombea wa ubunge na udiwani katika kata mbalimbali




Aidha  ameongeza kuwa  jumla ya vyama vyenye wagombe

kwa jimbo la dimani Zanzibar  ni 11 walioteuliwa kugombea ni 11 ambao wote ni wanaume kwa upande wa udiwani katika halmashauri 20 za Tanzania bara, vyama vyenye wagombea ni 13 jumla ya wagombea wa nafasi udiwani ni 72 kati ya wagombea hao wanawake ni 5 na wanaume ni67, hadi sasa pingamizi zilizokatwa ni sita ambapo tano ambapo tano zimekatwa  kwenye kata ya ihumwa manispaa ya Dodoma na moja katika kata ya isegehe halmashauri ya mjini wa klahama.

Aliongeza kuwa kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi, kampeni zinaanza tarehe 23/12/2016  hadi 21/1/2016 ambapo  kamati za maadili zitaundwa katika ngazi mbali mbali na zitakuwa na jukumu la kusimamia utekelezaji wa maadili katika kipindi chote cha kampeni.