WANAHARAKATI WAIBUKA NA KUDAI KATIBA MPYA,THRDC WAKOLEZA MOTO,SOMA HAPO KUJUA
WAKATI Rais John Magufuli akisema serikali yake
hataliweka kipaumbele zoezi la Katiba mpya kwa kile anachodai anataka kujenga
nchi kwanza.
Nao Mtandao
wa Haki za Binadamu Tanzania THRDC kwa kushirikiana na wadau wengine wa katiba
nchini wameamka na kufufua upya mchakato huo ambapo kwa madai yao
wamesema kuuwa mchakato ulisitishwa baada ya kutokea pande mbili zilizovutana
yaani walioikubali na walioipinga katiba pendekezwa
Akizungumza
na Waandishi wa Habari mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam baada ya
kumalizika kwa mjadala wa kitaifa kuhusu namna ya kufufua mchakato
upya Rais wa Chama cha Wafanyakazi Nchini TUCTA, Gratian Mukoba
ameeleza kuwa ni muda muafaka kwa asasi za kiraia kubeba agenda
mpya ya uandikwaji wa katiba bora ya Tanzania itakayolenga kuleta ustawi kwa
Taifa na Wananchi kwa ujumla.
Aidha,
Mukoba amefafanua kuwa ili wananchi waweze kujitokeza kwa wingi kuipigia
kura za maoni katiba pendekezwa, ni vyema muafaka wa kitaifa utawawezesha
wananchi wote kuungana na kuwa na maamuzi yanayofanana yatakayowaongoza kwenye
zoezi zima la upatikanaji wa katiba mpya ukapatikana kwani kwa kufanya hivyo
kutaondoa uwepo wa makundi ambayo yanakinzana.