Zinazobamba

ELIMU YACHANGIA KUPUNGUA MAUAJI YA ALBINO,SHIRIKA LA UNESCO LAJA NA UTAFITI HUU,SOMA HAPO KUJUA

Dk. Possi
ELIMU iliyotolewa na Serikali pamoja na Viongozi wa Dini imetajwa kuchagia kupungua mauji ya watu wenye ulemavu wa Ngozi (Albino).Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.

Kwa mujibu wa Utafiti uliofanywa na  Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)  katika Wilaya nne za Mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Sengerema, Misungwi, Msalala na Bariadi ambazo hapo mwanzo zilikuwa zinakithili kwa vitendo hivyo imeonyesha kupungua kwa hali hiyo.

http://mtembezi.com/wp-content/uploads/2016/11/ZULMIRA-UNESCO.jpg

Hayo yamebainishwa leo jijini dare s Salaam na Naibu Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Dk. Abdallah Possi amesema elimu pekee kwa wanachi ndio nguzo sahihi itakayopelekea mabadiliko na sio kuwatenga watuhumiwa wa mauaji wa Albino.

Aidha ameongeza kuwa katika masuala yanayoigusa jamii watu wengi wanahitajika kufanya kazi kwa pamoja pasipo kuiachia serikali pekee kwani watu wenye ulemavu wa ngozi wanapatikana katika jamii zote.
 “Jamii zikibadili fikra kuwa mtu yuko tofauti hakutakuwa na ubaguzi wowote kwani mwenye ulemavu anaweza kufanya kazi sawa na mtu mzima iwapo atajengewa mazingira rafiki” amesema Possi

Kwa upande wa UNESCO kupitia Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Zulmira Rodrigues amesema UNESCO imnatambua kila mwanadamu ana haki ya kuishi kama binadamu wengine na kupitia utafiti wao ambao uliambatana na kutoa elimu wanaamini kuwa ni muda wa jamii kushirikiana ili kutokomeza vitendo vya kikatili kwa maalbino.

“UNESCO imeamua kujihusisha sana na hili jambo na kujitahidi kutoa elimu kwa jamii, tumeanza kulifanyia kazi jambo hili la kikatili kwa maalbino na mashambulizi ambayo wamekuwa wanakutana nayo sababu ya imani za kishirikina ambazo ni kinyume na haki za kibinadamu,

“Utafiti huu utaweza kusidia kumaliza vitendo vya kikatili kwa watu wenye ualbino, kila mtu ana haki za kimsingi na hilo ndilo ambalo UNESCO inalisimamia, na katika kufanikisha hili kila mtu katika jamii kwa nafasi yake ana wajibu wa kushiriki kumaliza vitendo hivi, ni lazima kushirikiana kumaliza jambo hili,” amemalizia kusema  Rodrigues

Nandera Mhando ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni mmoja kati ya waliofanya tathmini hiyo ambapo amebainisha kuwa lengo kubwa la utafiti huo lilikuwa ni kuondoa ukandamizaji, uonevu na unyanyasaji katika jamii juu ya watu wenye ulemavu wa ngozi.