Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wamesemauchumiwa nchi unayumba, huku mawaziri walioteuliwa na Rais Dk.
John Magufuli wanaogopa kumweleza ukweli kiongozi huyo kuhusu hali ngumu ya
maisha inayowakabili wananchi.
Kutokana na hali hiyo, wamesema ipo haja kwa
Serikali kujitafakari na mipango yake mingi ambayo imekuwa na ugumu katika
utekelezaji wake.
Akichangia hotuba ya Mapendekezo ya Mpango wa
Maendeleo ya Taifa ya 2017/18 na Mwongozo wa Kuandaa Bajeti, iliyowasilishwa na
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango bungeni jana, Mbunge wa Nzega
Mjini,HusseinBashe(CCM), alisema hotuba ya waziri huyo haina jipya
ila imerudia mambo yaliyopita ya mwaka 2015/16, huku akihisi nchi hii ni ya
watu wa hali ya juu pekee.
Alisema kuwa Waziri Mpango alitakiwa kuichambua
ripoti iliyotolewa na Benki ya Dunia (WB) Oktoba 20, mwaka huu ambayo
inaonyesha uchumi wa nchi umezidi kuporomoka hadi kushika namba 139 duniani. Bashe alisema kilichowasilishwa na Waziri Mpango
ni tofauti na hali halisi ya maisha ya kawaida ya wananchi waliopo mitaani.
“Waziri wa Fedha usirudie uliyoyafanya 2016/17,
nalisema kwa sababu angalia vitabu vyake hapo, nchi hii si ya Executive Only
(si ya watu wakubwa pekee). Unakuja na kitu kilekile, eti eneo la kimkakati
Kurasini, huku unataka kuua Kariakoo ili Wachina watumie ile nafasi. “Jamani hatuwezi kwenda hivyo, boresheni Kariakoo
ili mruhusu hawa waswahili walipe kodi, tuacheni kabisa dhana mbaya.
“…Sijui kwa kuwa wewe hukuomba kura na hujui hali
ngumu iliyopo mitaani, vijijini fedha hakuna halafu unakuja hapa kusema
tunatekeleza. Waziri wa Fedha asipochukua tunayomshauri, tuna jukumu la
kuungana bila kujali itikadi zetu humu ndani bungeni,” alisema Bashe.
Alisema ni lazima waziri aangalie sheria za nchi
kama zinavutia wawekezaji wote na si wa nje peke yao. “Ninashangaa sana katika taarifa ya waziri,
anasema mazingira na hali ya hewa itakuwa nzuri huku taarifa za Mamlaka ya Hali
ya Hewa Tanzania (TMA), zinasema kuna ukame. Leo hali ya hewa kwa nchi jirani
unasema ni nzuri si kweli, kwa 2017/18 nchi zinazotuzunguka zina hali mbaya ya
chakula na hata taarifa ya TMA inasema hivyo,” alisema
WABUNGE WA CCM WACHARUKA,WAIBUKA NA KUIVAA SERIKALI YA MAGUFULI,YASHTUKA NA UGUMU WA MAISHA KWA WATANZANIA,SOMA HAPO KUJUA
Reviewed by Unknown
on
19:39:00
Rating: 5