UKAME KUITIKISA NCHI TENA,TMA YATABILI HALI HIYO,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
MAMLAKA ya Hali ya hewa nchini (TMA) Itabili
hali ya ukame takribani mikoa yote kutokana na kutokuwapo na mvua katika mwezi huu Novemba.
Hata Hivyo,Maeneo ya mikoa ya Kanda ya ziwa pekee ndio yanatarajiwa kuwa na mvua kiasi.
Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na
Mkurugenzi wa mkuu wa (TMA)Dkt Agnes Kijazi wakati wa mkutano na waandishi wa
habari ambapo amesema hali hiyo ya kutokuwa na mvua imetokana na upugufu
mkubwa wa unyevunyevu unaonekana katika maeneo mengi ya nchi kutokana na
kuendelea kuwepo kwa viashiria vya
kupunguza mvua.
“Tumeona Lanina
na joto la bahari la chini ya wastani katika eneo la magharibi mwa
bahari ya Hindi ,na hii sababu ndio imechangia kuwpo kwa upungufu wa mvua
katika maeneo mengi ya nchi “amesema Dkt Kijazi.
Hata Hivyo,Dkt Kijaza amewataka Wakulima pamoja na
Wafugaji kujiandaa na hali hiyo kwa kuhakikisha wanatunza akiba ya maji iliyopo
.
Amesema licha ya Utabili huo kuonyesha kuwapo kwa mvua chache (chini ya
wastani) kuna uwezekano wa matukio ya vipindi vya mvua kubwa pia kunaweza kutokea.