MADUDU YA KUTISHA YABAINIKA SHIRIKA LA POSTA,SOMA HAPO KUJUA
Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania
(TPC) imebaini madudu lukuki, ikiwamo mikataba mibovu, idadi kubwa ya
wafanyakazi wenye elimu ya chini, rushwa na kuajiri kwa upendeleo.
Akizungumza na wanahabari jana, mwenyekiti wa bodi
hiyo, Dk Haruni Ramadhani alisema shirika linakabiliwa na “maradhi” mengi
ambayo kama hayatashughulikiwa ipasavyo yanaweza kusababisha malengo
kutotekelezwa kwa ufanisi.
Kutokana na madudu hayo, bodi imeipa miezi sita
menejimenti ya TPC kurekebisha kasoro hizo na kinyume na hapo, hatua kali za
kisheria zitachukuliwa.
“Tumebaini Shirika la Posta lina uwezo
na fursa kubwa kama tutaitumia vizuri kuchangia Pato la Taifa. Ni shirika
ambalo limesambaza huduma zake toka ngazi ya Taifa, kata na vijiji. Posta ina
mizizi mingi mikubwa na imara,” alisema.
“Kinachokosekana ni utashi na kujituma,
ubunifu na utendaji kazi kwa weledi na umakini. Lazima sasa tubadilike, tuache
kufanya kazi kwa mazoea, uzembe, ubinafsi, ufisadi, wizi na rushwa. Vitu hivi
lazima tuambizane ukweli bila kuoneana aibu. Havina nafasi tena Posta,” alisema.
Mikataba Mibovu
Dk Ramadhani alisema wakati bodi hiyo ikiendelea na uchunguzi, imebainika shirika hilo liliingia mikataba mibovu ukiwamo ule wa kati ya TPC na kampuni ya Wande Printing and Packaging.
Katika mkataba huu, bodi ilibaini kuwa Wande Printing and Packaging walipangisha jengo la ghorofa tatu (mali ya shirika) kwa Sh1.8 milioni kwa mwezi, kwa muda wa miaka mitatu ambayo ni sawa na Sh64.8 milioni.
Dk Ramadhani alisema wakati bodi hiyo ikiendelea na uchunguzi, imebainika shirika hilo liliingia mikataba mibovu ukiwamo ule wa kati ya TPC na kampuni ya Wande Printing and Packaging.
Katika mkataba huu, bodi ilibaini kuwa Wande Printing and Packaging walipangisha jengo la ghorofa tatu (mali ya shirika) kwa Sh1.8 milioni kwa mwezi, kwa muda wa miaka mitatu ambayo ni sawa na Sh64.8 milioni.
Alisema baadaye, mwekezaji alifanya ukarabati wa
jengo kwa Sh398 milioni, hivyo ili kufidia fedha hizo, mkataba huo ulieleza
Wande Printing and Packaging itakaa kwenye jengo hilo bila kulipa kwa miaka 20
ili kufidia fedha zake.
Mwenyekiti huyo alisema mkataba mwingine ni kati ya
TPC na kampuni ya Universal G & G ambao ulihusisha upangishaji wa jengo
lililopo kitalu namba 416 Block G, Ubungo. Alisema katika mkataba huo Universal
G & G na TPC waliingia mkataba wa kudumu na TPC ina hisa asilimia 25 na
Universal asilimia 75.
Kaimu Posta Masta wa TPC, Fortunatus Kapinga alisema
waliingia kimakosa mkataba wa jengo la Posta lililo karibu na Mawasiliano
Tower, na sasa wapo kwenye utaratibu wa kuzungumza na mwanasheria wa kampuni.
Pamoja na mikataba mibovu, Dk Ramadhani alisema baadhi ya watumishi wa shirika hilo wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya rushwa kwa kufanya malipo hewa kwa wastaafu wa Shirika la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wakitumia mfumo wa Post Giro.
Pamoja na mikataba mibovu, Dk Ramadhani alisema baadhi ya watumishi wa shirika hilo wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya rushwa kwa kufanya malipo hewa kwa wastaafu wa Shirika la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wakitumia mfumo wa Post Giro.
Post Giro ni mfumo wa kizamani wa malipo kutoka
benki moja kwenda benki nyingine na mlipaji ndiye huidhinisha malipo
yote.
Mwenyekiti huyo aliyataja madudu mengine waliyobaini
ndani ya shirika hilo kuwa ni kuwepo na tabia ya kupeana ajira kwa upendeleo,
kupandishwa vyeo kwa rushwa, fedha au rushwa ya ngono.
“Kwa mfano vijana walioteuliwa na ofisi
ya General Manager, Corperate Resource Management baadhi yao wana dalili za
kujihusisha na rushwa. Mfano watumishi waliokuwa na vyeti feki wengi wao
walisaidiwa kuviondoa katika majalada yao,” alisema.
Pamoja na madudu hayo mwenyekiti huyo alisema
wamebaini ufanisi unadorora kwa kuwa zaidi ya wafanyakazi 120 wana elimu ya
darasa la saba na zaidi ya 1,000 wameishia kidato cha nne.
“Wale wote wenye tabia ya wizi,
umangimeza, rushwa, ubadhilifu na ufisadi hawana nafasi,”
alisema.
Dk Ramadhani alisema shirika hilo linasuasua
kutokana na wingi wa madeni na hadi Juni, 2016 lilikuwa linadaiwa Sh20.5
bilioni. Kati ya fedha hizo, Sh16 bilioni ni makato ya wafanyakazi yanayotakiwa
kwenda Mamlaka ya Mapato (TRA).
Pia, alisema TPC inaidai Serikali Sh5.5 bilioni,
taasisi za umma Sh1.9 bilioni, watu binafsi Sh1.8 bilioni na hivyo kulitaka
kuongeza juhudi katika kukusanya madeni.