LOWASSA ATESA CCM,WABUNGE WAZIDI LITAJA JINA LAKE,SOMA HAPO KUJUA
Edward Lowassa bado angali vinywani mwa
wabunge japokuwa hayupo tena Bungeni .Jina lake jana limeibua mjadala bungeni
wakati wabunge walipotoleana maneno makali kuhusu waziri huyo mkuu wa zamani.
Sakata hilo limetokea wakati Bunge la Jamhuri ya
Muungano lilipokuwa likijadili Muswada wa Huduma ya Habari ambao ulipitishwa
jana licha ya kupingwa vikali na kambi ya upinzani na wadau wa habari.
Lowassa amelizua tafrani bungeni baada ya wabunge
wawili kurushiana maneno kuhusu taarifa zake tofauti zilizokuwa zikiandikwa na
vyombo vya habari kiasi cha kusababisha mwenyekiti wa Bunge aingilie kati.
Akichangia muswada huo, mbunge wa viti maalumu
(CCM), Amina Mollel amerejea sakata la zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura
iliyopewa kampuni ya Richmond Development ya Marekani ambayo ilibainika baadaye
kuwa haikuwa na uwezo. Sakata hilo lilitokea wakati Lowassa akiwa Waziri Mkuu.
“Mimi naomba ninukuu baadhi ya vichwa
vya habari ambavyo vilitumiwa katika magazeti,”
amesema Mollel, ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari.
Mollel ametaja mfano wa gazeti lililoandika
“Lowassa anajua uzalendo au ni machozi ya mamba” na kichwa kingine cha
habari cha gazeti hilo kilichosema “Lowassa Hasafishiki” na kingine
kilichosema “Lowassa karibu Chadema”.
“Kuna haja ya kuwa na waandishi ambao
leo hii wanaandika habari kwamba mtu huyo ni mbaya lakini kesho hiyo hiyo uongo
huo unabadilika na kuwa ukweli?”amehoji Mollel.
Amesema Taifa linahitaji kuwa na sheria kama hiyo
ambayo inaweza kulinda taaluma ya waandishi wa habari, hivyo kupitishwa muswada
huo ni kwa manufaa ya wanahabari.
Maneno hayo kuhusu Lowassa yakamfanya mbunge wa
Konde (CUF), Khatib Said Haji kusimama na kutumia methali inayosema “ukienda
kwa wenye chongo, ufumbe macho ili ufanane nao japokuwa unaona”.
“Leo kituko cha karne hii ni pale
anaponyanyuka mbunge wa CCM ndani ya Bunge akatulaumu eti sisi (wabunge wa
kambi ya upinzani) kwa sababu tunampenda Lowassa. Hiki ni kituko cha karne,” amesema.
“Rudini kwenye kumbukumbu ya Mkutano
Mkuu wa CCM kuhusu kale kawimbo katamu. Kweli?” amesema
na kufanya wabunge wengine wa upinzani kuanza na kuimba “tuna imani na
Lowassa”.
Jina la Lowassa limekuwa likiibuka kwenye vikao
mbalimbali na katikati ya mwaka lilikuwa gumzo kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa
CCM ulioitishwa kwa ajili ya uchaguzi wa mwenyekiti mpya wa chama hicho,