Zinazobamba

SHIRIKA LA HAKI YA ELIMU LAIPONGEZA SERIKALI YA MAGUFULI,SOMA HAPO KUJUA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh69reoZ5EQU-PrZ4kj2mUdKuQu919zsgXUzbYJtxCzAG2yWiIae-vejtma35T6tnq5ucEmXsZPaAYpMsj9pteioL1dAT_p2FSIesNU76T6O7johH1gXvEDaUiU57JC_5UH2wlmKRe37S7c/s1600/unnamed+%25281%2529.jpg
Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Elimu,John Kalage katikati akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya kuishauri Serikali kuharakisha uundaji wa bodi ya kitaalamu ya Walimu ili kusaidia kuweka na kubaini viwango bora vya taaluma ya Ualimu.Kulia ni Meneja Habari na Utetezi-Haki Elimu,Elisante Kitulo,Kutoka Kushoto ni Maneja Udhibiti Ubora Haki Elimu,Robert Mihayo.
NA KAROLI VINSENT
Shirika lisilo la Kiserikali linalojihusisha na Elimu nchini, (HAKI ELIMU) limeelezwa kufurahiswa na  serikali ya awamu ya tano  kwa hatua yake ya kuondoa mamlaka ya usimamizi wa elimu wa ngazi ya stashahada kutokaka Baraza la elimu ya ufundi nchini (NECTA) na kurufisha wizara huku ikiwa chini ya ungalizi wa Baraza hilo.
Wamesema hali hiyo itasaidia wizara itakuwa ikitoa maelekezo  ya sifa ya kujiunga  na mafunzi ya elimu na kusaidia kuondokana na ujanja janja uliopo.
 Hata hivyo Shirika hilo  limeishauri Serikali kuharakisha uundaji wa bodi ya kitaalamu ya Walimu ili kusaidia kuweka na kubaini viwango bora vya taaluma ya Ualimu.


Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam mkurugenzi wa Haki ya elimu,John Kalage amesema hatua hiyo ya serikali imekuja baada mapema mwezi huu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ufundi kutoa waraka Na.5 wa Mwaka huu 2016 unaoleta Mabadiliko kadhaa katika program za Mafunzo ya Ualimu nchini.

Amesema miongoni mwa Mabadiliko hayo ni kwenda mamlaka ya usimamizi wa Elimu ngazi ya Cheti na stashahada kutoka NACTE na kuyarudisha wizarani chini ya uangalizi wa baraza la mitihani NECTA.

Kalage amesema kuwa kwamujibu wa waraka huo programu za Mafunzo ya Ualimu zitakuwa Astashahada Cheti, na stashahada , Diploma Mafunzo taraji ya stashahada ya juu ya Elimu sekondari yalikuwa yakitolewa kuanzia Mwaka wa masomo 2014/15 yamesitishwa.

"Wizara ya Elimu ndio itakuwa ikitoa maelezo ya sifa za kujiunga na Mafunzo ya Ualimu, Necta itakuwa inasimamia Mafunzo ya Ualimu huku ikitahini na kutoa tuzo", amesema Kalega.