Zinazobamba

TUHUMA ZA RUSHWA KWA WUZAJI SHISHA ZAMTIKISA KAMANDA SIRRO,SASA AAMUA KUWAANGUKIA WANANCHI,SOMA HAPO KUJUA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiG9oOrPKT0bI47k7n-Xig_Ga3-ErtXVr60HrCqoCf3imkXVmaj4VNNis88pT6JWi2NmXLBi19DynufR3khRLDaoODrE2mQAeatRpVgW9cdc7WUZJOSC0lPwcV6l4DIjwM2HMo2FPcmKUN-/s1600/unnamed.jpg
Kamanda wa jeshi la  polisi kanda maalumu mkoa wa Dar es salaa,Saimon Siro amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuweza kuwabaini wauzaji wa madawa ya kulevya aina hiyo.

Kauli hiyo ya Kamishna Sirro inakuja ikiwa ni wiki moja kupita baada ya mkuu wa mkoa wa dar es Salaam,Paul mkonda kumtuhumu Sirro kuwa amechukua rushwa ya milioni tano kutoka wauzaji wakubwa wa shisha ili apunguze kasi ya kuwakamata wauzaji hao,
Baada ya shtuma hizi jambo lilolifanya jeshi la Polisi Makau mkuu kumchunguza Kamanda haya pamoja na Kamanda wa polisi mkoa wa Polisi Kinondoni,


Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salam Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishna Simon Sirro amesema  zoezi hilo bado linaendelea ili kuwabaini wauzaji wa shisha.

Amesema  katika Wilaya ya Kinondoni  wamefanikiwa kuwakamata watu watatu na vielelezo,amesema watawapeleka mahakamani baada ya kupeleka vielelezo kwa Mkemia Mkuu wa serikali na taratibu za mahakamani zitaendelea.
‘’Opareshini dhidi ya shisha bado unaendelea na tunawaomba wananchi wa mkoa wa Dar es salaam waendelee kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili tuweze kuwabaini wauzaji wa dawa za kulevya aina ya shisha’’  amesema Kamanda Sirro