Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imesema haimuogopi kumwadhibu Mbunge wa
Singida Mashariki, Tundu Lissu na imemuonya tabia yake ya kushindwa
kufuata taratibu za kisheria anapokuwa na udhuru siku kesi yake inapopangwa
kusikilizwa.
Kadhalika imesema Lissu anatakiwa kuwa mfano wa kuigwa kwa jamii, mshtakiwa
huyo alishindwa kufika mahakamani mara tatu mfululizo kusikilizwa kesi yake na
wenzake watatu dhidi ya mashtaka ya uchochezi kupitia gazeti la Mawio.
Onyo hilo lilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya mahakama
yake kutoa amri ya kukamatwa Lissu Novemba 3, mwaka huu.
"Pamoja na nafasi yako uliyonayo kwa jamii lakini ujue kwamba mahakama
hatukuogopi labda upande wa Jamhuri ulioshindwa kuja kukukamata ... mahakamani
hakuna kuoneana bali taratibu za kisheria zinachukua mkondo wake" alisema
Hakimu Simba.
ifuatayo ni sehemu ya mahojiano kati ya hakimu na Lissu:
Hakimu Simba ; Awali ulikwenda Ujerumani bila kutoa taarifa mahakamani unadhani
tunakuogopa?
Lissu; Sina nia mbaya mheshimiwa hakimu nilipelekwa Ujerumani kwa dharula.
Hakimu Simba ; Je, kesi ya Uchaguzi wa Jimbo la Bunda nayo ilikuwa ni dharula?
Lissu; Mheshimiwa hakimu nilipotoka Ujerumani nilikuta kesi ya Bunda imepangwa
kusikilizwa na ilikuwa na muda maalumu, niliandika barua Hakimu Mfawidhi wa
mahakama hii ya Kisutu na nakala nilielekeza kwa upande wa Jamhuri sina nia ya
kuidharau mahakama.
Hakimu; Kutokana na nafasi yako katika jamii ujue kwamba mahakama hatukuogopi
labda upande wa Jamhuri ulioshindwa kukukamata na kukuweka chini ya ulinzi.
MBUNGE LISSU NI PASUA KICHWA MAHAKAMANI,HAKIMU AMUONYA,SOMA HAPO KUJUA
Reviewed by Unknown
on
18:55:00
Rating: 5