YESU, IMAM HUSEIN WANAFANANA KWA HAYA
Kiongozi Mkuu wa kiroho wa Waislam wa dhehebu la Shia ITHNASHERIYA Tanzania Sheikh HEMED JALALA akizungumza na wanahabari mapema Leo Jijini Dar es salaa. |
Imeelezwa kuwa Yesu na Imaam Husein (Mjukuu wa Mtume) wanafanana kwa harakati zao za kuamrisha mema, kukatazana maovu jambo ambalo kila mmoja alijitoa kuhakikisha mema yanatendeka ili dunia kuwa sehemu salama ya Kuishi.
Hayo yamesemwa leo
Jijini Dar es salaam na Kiongozi Mkuu wa kiroho wa waislam wa dhehebu la Shia ITHNASHERIYA Tanzania Sheikh HEMED JALALA wakati
wa semina maalum kwa ajili ya kujadili kwa pamoja Jitihada za wawili
hao katika kuleta Amani na utulivu pamoja na kuleta haki na usawa
Duniani.
Sheikh Jalala amesema watu hao ni mfano wa kuigwa kwa sasa hii
ikiwa ni semina pia ya kuadhimisha Arobaini ya Mjukuu huyo wa mtume
Mohamad (s.a.s)
Sheikh Jalala amesema
kuwa Semina hiyo inalengo la kuweka ulinganisho kwa watu hao wawili ambao ni
Imam Husein na Nabii Isaa ambaye ni Yesu ambao wote kwa pamoja walikuja Duniani
kwa ajili ya kuleta mabadiliko kwenye Dunia katika Nyanja mbalimbali zikiwemo
Haki kwa watu wote,na kutetea wanyoonge na kufanya watu wapendane katika Jamii.
Semina Ikiendelea |
Ameongeza kuwa ni
wakati wa watanzania kuacha mambo mambo mabaya na kuanza kufanya matendo ya
kiumpendaza mungu yakiwemo kupendana,kupinga dhuluma,na kutetea wanyonge ili
kuhakikisha kuwa wanawaenzi viongozi hao wa Kidini waliopambana kwa ajili ya
dunia.