BIFU LA KUSAGA , RUGE WA CLOUDS NA MSANII JAY D MAHAKAMA YAMTIA HATIANI JAY D,SOMA HAPO KUJUA
Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni imemkuta na hatia mwanamuziki
Judith Wambura maarufu Lady Jaydee kumkashifu Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds
Media Group, Joseph Kusaga pamoja na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa
Clouds Media Group Ruge Mutahaba.
Hukumu hiyo imesomwa mahakamani hapo kufuatia kesi
iliyokuwa imefunguliwa na viongozi hao wawili wa Clouds Media Group wakimtuhumi
Judith Wambura kuwakashifu na kuwaharibia taswira zao na kampuni yao katika
jamii.
Awali mahakama hiyo ilipanga kusoma hukumu ya kesi
hiyo ya madai Oktoba 13 mwaka huu lakini Hakimu Lyamwike aliiahirisha hadi
Novemba 2 mwaka huu kwa maelezo kuwa hakuwa amemaliza kuiandikia hukumu.
Katika kesi ya msingi, Joseph Kusaga na Ruge
Mutahaba waliiomba mahakama itamke kuwa maneno yaliyotolewa na Judith Wambura
kubitia blog yake ni kashfa na yanaathiri taswira yao katika jamii, pia
mahakama imuamuru aombe radhi kupitia vyombo vya habari na alipe fidia kutokana
na madhara ya jumla kwa jinsi mahakama itakavyoona inafaa.
Judith Wambura aliandika waraka katika blog yake na
kwenye baadhi ya magazeti uliokuwa na kichwa cha habari “Wosia wangu ikitokea
nimetangulia kufa kabla ya Ruge na Kusaga.”
Wakati akijibu shtaka hilo, Wambura ambaye alikuwa
mtetezi pekee wa upande wake alikiri kuandika waraka huo, hivyo mahakama
imemtaka aombe radhi kwenye chombo cha habari chenye coverage kubwa hapa
nchini na ikiwezekana duniani pia