WAZIRI MAHIGA AISIFU UN,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikikiano wa Afrika Masharikia,Balozi Dkt Augustine Mahiga |
NA KAROLI VINSENT
WAZIRI wa Mambo ya nje na Ushirikikiano wa Afrika Masharikia,Balozi Dkt Augustine
Mahiga amesema Tanzania imepata mafanikio makubwa na uhusiano na Shirika la
Umoja wa Mataifa (UN) katika kufanikisha
kudumisha amani na kuwaletea maendeleo wananchi .
Balozi Dkt Mahiga
ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa
habari kuelekea siku ya umoja wa Taifa Duniani ambayo inasherekewa kila mwaka octoba
24 na mwaka huu Shirika hilo linatimiza miaka 71 tangu kuanzishwa kwake.
Amesema Tangu Tanzania kujiunga uwanachama na Shirika hilo
limepata mafanikio makubwa ikiwemo kuletewa maendeleo mbali mbali inayotokana
na misaada inayotolewa na shirika hilo pamoja na kudumisha amani.
Amedai kuwa shirika hilo linasimamia na kuhakikisha nchi
zote ziliko nchini ya umoja wa Mataifa yanahakikisha yanadumisha amani jambo
analodai linastahiri kupongezwa kwa shirika hilo.
Ameongeza kuwa kwa sasa serikali itahakikisha inadumisha
uhusiano na shirika hilo kwani wamebaini linamchango mkubwa katika kuwaletea
maendeleo wananchi wake pamoja na kudumisha uhusiano na mataifa makubwa.
Amekumbusha kuwa UN imeleta mchango mkubwa wakati wa
kufanikisha nchi kupata uhurukwa kudai kuwa shirika hilo lilikuwa linatoa nguvu kwa Taifa
kuhakikisha tunajikomboa na kupata
uhuru,
Kwa Upande wake Kaimu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa
nchini,Bi Chansa Kapaya amesema kwa sasa Tanzania na umoja wa mataifa zimekuwa
na ushirikiano kwa miaka mingi,
Amesema ni wakati kubadilika kwa Tanzania kutokana na misaada
mbali mbali inayotolewa na umoja
mataifa huku akitaka kukidhi haja
mpya husasani kwa kipindi cha Taifa linapoelekea uchumi wa kati.