VYETI FEKI VYAMTESA WAZIRI MWIGULU.,SOMA HAPO KUJUA
Wakati
Serikali ikitangaza msako kwa watu walioghushi vyeti na kutumia majina ya watu
wengine, Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi, Mwigilu Nchemba, ameibuka na kutoa
ufafanuzi wa utata wa majina yake.
Hatua
hiyo imekuja baada ya kuibuka kwa mjadala wa usahihi wa majina yake pamoja na
kuhusishwa kughushi vyeti ya elimu.
Katika
andiko lake aliloliweka jana katika mitandao ya kijamii ambalo baadaye
lilithibitishwa na mmoja wa wasaidizi wake, Mwigulu alisema watu wanaoandika
historia yake hawamjui kwani uhalisia alikuwa akiitwa Lameck Madelu Mkumbo,
sasa Lameck si jina la Kinyiramba na Madelu si jina halisi la baba yake bali la
utani.
“Ni vema kuweka rekodi sawa, kwanza anasema (aliyeandika) nilikuwa
naitwa Lameck Madelu Mkumbo, sasa moja Lameck sio jina la kinyiramba, na Madelu
sio jina halisi la baba bali ni utani kuwa ana ndevu nyingi, yaani ni mandevu.
Ndiyo maana hata kwenye ubunge nililiongeza tu kama a.k.a ili watu, hasa wazee
wanifahamu, hili haliko kwenye vyeti.
“Hili la Lameck siyo jina la Kinyiramba ni jina la daktari
aliyenipokea zahanati iliyopo Kijiji cha Mukulu, daktari tunaita hivyo, lakini
ni nesi ndiye aliyekuwa anaitwa Mwigulu na jina la kizungu Lameck.
“Mimi nilipelekwa hospitali nikiitwa Mugulo na jina la ukoo kwa
watoto wote wa kiume ni Shumbi, ambalo hata hivyo wanatumia wazee tu, wanaojua
Kinyiramba hilo ndio jina la Kinyiramba,” alisema Mwigulu na kuongeza:
“Mama yangu aliulizwa jina akanitaja kwa muuguzi (nesi) akamwambia
mama unamwitaje jina hilo hakuna lingine, mama akamwambia hakuna labda mtaje
wewe, basi jamaa akajitaja,” alisema.
Alisema
suala hilo ni jambo la kawadai hasa kwa kijijini kwani familia inakuwa na
watoto wengi hadi majina inakuwa si jambo la kujali.
“Hata pale kijijini kuna wengine waliotajwa majina ya waganga wa
kienyeji wazee walikopewa dawa, majina ya manesi, matabibu kama mimi, majina ya
walimu,” alisema.
Akizungumzia
maisha yake ya elimu, alisema aliacha shule kwa mara ya kwanza mwaka 1984 baada
ya kuanza na kaka yake aliyemtaja kwa jina la Jugulu.
Mbunge
huyo wa Iramba alisema kutokana na hali hiyo, baba yao aliwataka wapeane zamu
ya kwenda shule hali iliyomfanya aache shule.
“Mwaka 1985, nikaachia darasa la tano nikaenda kuchunga miaka kama
miwili. Nikarudi tena baada ya mifugo kuanza kufa sana, mzee akashauriwa
awekeze kwenye elimu. Walimu walikuwa wanashinda nyumbani kumsihi anirudishe
shule, ndiyo nikarudi na nikachukua majina ya daktari.
“Mtu asichanganye kuona ni udanganyifu, mimi sijachukua vyeti vya
mtu. Nimefanya mitihani tena kwa kupiga na picha za passport ili mtu asitumie
haki ya mtu mwingine aliyefaulu na mpaka sasa naona ni struggle (kupambana) za
mfano, kuwa nilisoma kwa mazingira ya kutoka kuchunga na kurudishwa shule na
kufaulu mwenyewe,” alisema Mwigulu.
Waziri
huyo alisema kwa anayetaka kuthibitisha maelezo aliyotoa, anaweza kuwauliza
aliosoma nao shule ya msingi.
“Comrades kwa mawazo yangu kosa ni mtu kuchukua nafasi ya mtu
aliyefaulu na kwenda yeye, hapo ni kuiba haki ya mtu. Najua hii ilikuwa
ikitokea baadhi ya maeneo, mtu anafaulu ila anakuwa hataki kwenda shule au
amefariki then anakwenda mwingine. Mimi sijawahi chukua nafasi ya mtu.
“Halafu watu wanasema jina la mtu, labda kama wanamaanisha tofauti
na wizi wa jina kwani kila mmoja hapo alipo ana jina la mtu, yaani atakuwa John
wa Biblia, Mohamed wa Quran, litakuwa la babu, bibi la mganga, daktari, rafiki,
kiongozi au hata la tukio.
“Nijuavyo jina unakula kiapo tu kama sio la kwako kisheria na
unatumia, na hata sasa nikitamani jina jipya nakula kiapo na kutangaza katika
Gazeti la Serikali na lisipopingwa ndiyo linakuwa jina langu jipya.
“Hoja ni kama mtu kapora cheti cha mtu, kapora nafasi ya mtu
mwingine aliyefaulu akaenda kuisomea yeye. But, things do change pia kutokana
na nyakati na mazingira,” alisema Mwigulu.