WATU MILIONI 1.6 HUFARIKI KILA MWAKA KUTOKANA NA MAGONJWA YA JAMII PNEUMOCOCCAL,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Mkurugenzi wa Sayansi AMP, Dr. Bradford
Gessner akizungumza wakati wa Mkutano wa Kanda ya Afrika wa Magonjwa
yatokanayo na Pneumococcal kwaajili ya Kuangalia mafanikio katika miaka 5 tangu
kutambulishwa kwa chanjo ya PCV13 na kujadiliana mustakabali wa miaka mitano
ijayo mkutano huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo.
IMEELEZWA kuwa kiasi cha watu milioni 1.6 hufariki
duniani kila mwaka kutokana na Magonjwa
ya jamii ya Pneumococcal.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Kwa Mujibu wa Taarifa ya Shirika la Afya Duniani
(WHO) limeyataja magonjwa hayo ni nimonia/ homa za mapafu, homa ya uti wa mgongo
na maambukizi ya damu).
Mkurugenzi wa Sayansi AMP, Dr. Bradford
Gessner ametoa taarifa hiyo leo Jijini dare s Salaam wakati wa Mkutano wa
Afrika wa kuhusu magonjwa ya pneumococcal ,mkutano huo ulio kusanya viongozi na
wasimamizi katika sekta ya chanjo kutoka katika nchi ambazo zimeshatambulisha
chanjo au zinazotaka kutambulisha chanjo
.
Amesema kwa sasa
ugonjwa huo umekuwa kasi sana katika nchi zinazoendelea,kwa sasa shirika
la (WHO) limedhamilia kutoa chanjo ili kuhakikisha tunauondokana kabisa na ugonjwa huu,kwa kutoa chanjo hizo.
“Kuwepo kwa taarifa za karibuni na pia
kubadilishana mafunzo ya mipango ya chanjo itawezesha washiriki kusaidia
maamuzi ya nchi kwa kutumia vithibitisho.”
“Lengo la msingi la Gavi ni kupunguza maradhi na
vifo kwa watoto wachanga kupitia chanjo na Pfizer inajivunia kuwa mshirika
ikijumuika na washirika wengine katika magonjwa ya pneumococcal kupitia soko la
awali la kujitolea ambalo linategemewa kuweza kuepusha magonjwa haya kwa watoto
milioni moja kufikia mwaka 2020,” amesema Heather Sings
Hata hivyo, Dr Gessner amesema Tangu Gavi ilipoanza kusapoti
chanjo ya PCV13 mwaka 2010, nchi 18 kutoka Africa wametambulisha chanjo hii
katika mipango yao ya chanjo na kinga. Kama jina lake lilivyo PCV13 inatoa
kinga dhidi ya vimelea 13 vinavyosababisha magonjwa ya pneumococcal.
Pichani ni Meneja wa Taifa wa Mpango wa Chanjo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dafrossa Lyimo akizungumza na waandishi wa habari mara ya kumalizika kwa mkutano huo, |
Kwa Upande wake Meneja wa Taifa wa Mpango wa Chanjo
kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dafrossa
Lyimo amesema kwa sasa Tanzania imekuwa ikinufaika kwa chanzo hizo kwa kuzitoa
kwa watoto wadogo wenye umri wa miaka 5
“Tumekuwa tukipokea chanjo kutoka shirika la GAVI ambazo tumekuwa
tukigawa nchi nzima ili kila mtoto aweze kupata, sisi tunachukua chanjo Milioni
1.9 kwa mwaka na takwimu zetu zinaonyesha watoto 97% wamekuwa wakipata chanjo
na kwasasa tunajiuliza jinsi gani tutakamilisha ifike 100”amesema Lyimo.
Amesema kuwa mkutano huo
utaweza kuwasaidia kuona ni jinsi gani wataweza kutokomeza kabisa magonjwa
yanayotokana na Pneumococcal na zaidi ugonjwa wa Nimonia licha ya takwimu
kuonyesha kuwa kwasasa Tanzania inafanya vizuri.
Hata hivyo,Bi Lyimo ameitaka jamii kupuuza taarifa
zinasema chanjo haipo kwenye hiyo haipo kwenye Hospitali husika kwa kutakiwa
kuwapeleka watoto wadogo ili wapate chanjo hiyo ili waweze kujikinga na
magonjwa hayo anayodai ni hatari sana.
Picha zaidi katika mkutano huo hizi hapa