MEYA WA UKAWA ILALA AMZUNGUMZIA HAYATI MWALIMU NYERERE KWA KINA,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Meya wa manispaa ya Ilala,Charles Kuyeko |
NA KAROLI VINSENT
Wakati kesho tarehe 14-10-2017, Tanzania inatimiza
miaka 17 baada ya kifo cha mwasisi wa Taifa hili,Hayati baba wa Taifa Mwalimu
Julias Nyerere kututoka Duniani.
Viongozi mbali mbali
wamekosoa hali ya sasa ya nchi kwa kusema matendo yanayotendwa na
wananchi pamoja na viongozi hayaendani na matendo aliyokuwa anayetenda Mwalimu
Nyerere enzi za utawala wake kwenye miaka ya 1961 hadi 1985.
Wamesema matendo hayo ni kuwa na uzalendo na Taifa,kubuni
mipango ya mendeleo pamoja na kupambana na maadui watatu,yaani ujinga,maradhi
na umasikini.
Meya wa Manispaa ya Ilala Jijini Dar es
Salaam,Charles Kuyeko amemzungumzia kwa kina Mwalimu Nyerere na matendo yake leo jijini hapa wakati
alipokuwa anszungumza na waandishi wa habari ofisi kwake, kuelekea siku ya
kesho.
Amesema kwa sasa Watanzania wamekosa uzalendo ambao
alikuwa ametuachia baba wa Taifa hili,
“Namfahamu Mwalimu Nyerere alikuwa mzalendo na nchi
yake na alitufundisha watanzania kuwa wazalendo na kuipenda nchi hii,ila kwa
sasa kumekuwa na mmonyoko mkubwa kwa watanzania kutokuwa na uzalendo,kuacha misingi
aliyotuwekea ya upendo na nchi,”amesema Kuyeko.
Kuyeko, amesema Mwalimu Nyerere aliwafundisha
watanzania katika kuipenda nchi yao ili kuweza kuiilinda na kuwafichua maadui wanchi
yetu ila amedai kwa sasa Watanzania wamekuwa wakifumbia macho waharifu na
kushindwa hata kuwalipoti kwenye Mamlaka husika hatua hiyo anaiita ni ya kukosa
uzalendo.
Meya huyo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Chadema ambaye anaungwa mkono na Vyama vinavyounda Umoja wa kutetea katiba ya
wananchi (UKAWA) amesema sanjari na uzalendo alikuwa nao Mwalimu Nyerere katika
utawala wake pia aliweza kutatua tatizo vijana kukosa ajira baada ya kuanzisha
viwanda,makampuni mbali mbali.
“Kipindi cha Mwalimu suala la ukosefu wa jajira
lilikuwa halipo,kwani Mwalimu alibuni ajira mbali mbali ikiwemo kuanzisha
Viwanda vingi,kulikuwa na viwanda vya kutengeneza nguo kila kona,pamoja na
kuanzisha Mashirika ya umma,”amesema Kuyeko,
Amedai hata hali ya wazazi kipindi hicho kuwapeleka
watoto shule ilianza kuwepo baada ya wazazi hao kuamini watoto wao wakimaliza kazi
watapata ajira kwenye viwanda na Makampuni Jambo analodai ni tofauti na sasa kwani watu wengi wanamaliza
vyuo vikuu wanakosa ajira kutokana na viwanda vingi kufa huku mashirika ya umma
yakiwa katika hali mbaya.
Pia meya huyo amezungumzia dhana ya utawala wa awamu
ya Tano chini ya Rais John Magufuli dhana ya “Hapa kazi tu” kwa kusema dhana
hiyo itatimia endapo wakifanya kazi kwa vitendo kama alivyofanya Mwalimu
Nyerere katika kulitumikia Taifa.
Pamoja na hayo,Meya huyo ambaye amesifika kwa kipindi kifupi
alichoingia madarakani ndani ya manispaa ya ilala kwa hatua yake ya kusimamia
vizuri mapato ya Halmashauri hiyo pamoja na kuhakikisha madiwani wanapitisha
bajeti yenye kuwajali wananchi, ameitaka Jamii kufuata yale mambo mazuri
aliyoyafanya mwalimu nyerere kipindi cha utawala wake.