TUKIO KUBWA LEO JIJINI DAR-SHEIKH JALALA AWAFUNDA WATANZANIA,SOMA HAPO KUJUA
.Mzungumzaji na Kiongozi Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania,Sheikh Hemed Jalala akizungumza na waandiishi wa habari wakati wa maandamano ya Amani ya kuadhimisha sikuu ya Ashura (Kifo cha Imman Hussein)Maandamano hayo yalianzia Ilala Boma Jijini hapa na kumalizikia Kigogo Post |
.Waandamanaji wakiwa kwenye maandamano hayo |
NA KAROLI VINSENT
WATANZANIA wametakiwa kuhakikisha wanafanya
matendo ya kumpendezesha mungu kwa kujitolea kuwasaidia watu wasiojiweza katika
jamii.
Pia wamehaswa kujitoa muhanga katika kupinga na kuyakataa mambo ya dhuluma,mauaji kwa watu wenye ulemav wa ngozi pamoja na vitendo vya ujambazi.
Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Kiongozi mkuu wa Waislam shia ithnasheria Tanzania,Sheikh Hemed Jalala wakati wa maandamano ya Amani ya kuadhimisha siku ya Ashura (Kifo cha Imman Hussein) maandamano hayo ambayo yalianzia Ilala Bomo Jijini hapa hadi Kigogo Post .
Sheikh Jalala amesema jamii inatakiwa kufanya mambo ambayo ni mema katika jamii kama aliyofanya Imman Hussein ambaye alijitolea katika kupinga mambo ya dhuluma na uonevu yaliyokuwa yanafanyika katika jamii.
“Dunia inalazimika kuitika wito wa Imman Hussein katika kufanya mambo mema,ila kuinusuru dunia iliyotapakaa damu kila kona,ambapo afrika mashariki ya kati ambapo imekuwa ikishudiwa watoto wakichijwa na kupeleke maelfu kukimbia makazi”’amesema Sheikh Jalala.
Kiongozi huyo wa Kiroho amesema kwa sasa jamii imekuubwa na vitendoo vihovu ambavyo amedai vimechangiwa na watu kutokuwa na hofu ya mungu.
Ameongeza kuwa Imam Hussein aliwafunza watu namna ya kupinga
ukandamizaji,dhuluma,katika jamii pamoja na kutetea haki za wanyonge hivyo ni
wakati wa wananchi wa Tanzania kuanza kufwata maneno yake na kuhakikisha kuwa
wanaenzi yale mema aliyoyaacha katika jamii.
Amedai kuwa matembezi ambayo wameyafanya leo
yalikuwa na lengo la kuwakumbusha watanzania kuwa na upendo umoja na mshikamano
kwa kila jambo katika jamii na pia kuwapa ujumbe waislam na wasio waislam juuu
ya mambo aliyoyafanya Mjukuu huyo wa Mtume,matembezi ambayo yemeanzia maeneo ya
ilala Boma na kuishia Msikiti wa Shia Kigogo.
Ameielekeza jamii kutobaguani kwa rangi dini wala kabila.